MWIGIZAJI nyota wa kike wa filamu za Bongo,
Salama Salmin 'Sandra' amefunguka na kukanusha uvumi uliowahi kuvuma
kuwa amepewa talaka na mumewe.
Sandra amedai kuwa uvumi huo ulikuwa kama mkosi kwani alipata ajali
ya gari na kupata majeraha jambo lililomfanya ashindwe hata kuweka wazi
kuhusu sakata hilo.
Sijawahi kuachwa na mume wangu wala kutengana naye hata kwa muda,
nilishangaa kusikia habari hizo, hadi sasa nipo katika ndoa yangu na
wanaojua ni familia yangu na majirani zangu ambao kila siku wananiona
nikiamka kwangu na mume wangu mpenzi, sijui aliyetengeneza hiyo
'scandal' (kashfa) alikusudia nini?,anasema Sandra.
Msanii huyo amedai kuwa kuna rafiki yake ambaye aliamua kumchafulia jina kwa lengo la kuvunja ndoa yake lakini hakufanikiwa kwani yeye bado yupo katika ndoa akiishi vema na wanaye wawili, Harith na Aqaam na mumewe na kuwataka watu waangalie maisha yao.

No comments:
Post a Comment