HAKUNA ubishi kwamba maisha ukiyapangilia ni mazuri sana, yatakupa
amani na kwa ujumla utatamani uendelee kuishi milele, usipokuwa makini
utaishia kujuta.
Uamuzi wako ndio hutengenezahatma ya maisha yako; je unavyoamua ni
sahihi? Kila mtu analo jibu. Ikiwa tayari uko kwenye uhusiano, na
unamkubalia mwanamume mwingine kwa sababu zozote, ni dalili kwamba akili
yako imekufa.
Katika maisha kuna watu wamekuwa wakilia kwa raha, wengine kwa taabu, wengine wamekuwa wakicheka bila hata kuchekeshwa mara nyingi ni kwa sababu wanatiwa raha. Je, mara ya mwisho kufurahi au kukaa na mwenzi wako na mkafurahi ni lini?
Jambo ambalo unapaswa kubaki nalo kupitia makala haya ni kwamba watu wanaingia kwenye uhusiano kwa ajili ya kusaka raha, sio kusaka watu wa kuwapiga makofi, si kusaka watu wa kuwatukana na kuwakosesha amani.
Hii ina maana kwamba kama uko kwenye uhusiano, fanya uwezalo kuhakikisha unamtia raha mwenzi wako. Kama hapati raha, ni suala la kukaa na kuangalia nini cha kufanya ili mwenzi wako aweze kuwa mwenye raha. Duniani tunapita, yanini kutendeana mabaya jamani?
Inasikitisha kwamba kuna watu wamekuwa wakianzisha uhusiano kwa raha, wanafanyiana mazuri mengi, wanapanga mikakati mingi mizuri, lakini inafikia wakati watu hao hao wanaanza kutiana shida, kutukanana, kupigana na kunyanyasana kwa namna moja ama nyingine.
TOFAUTI YA ELIMU, KIPATO
Hilo swali nimekuwa nikiulizwa na wasomaji wengi mno, huwa sipendi kulizungumzia.
Ukweli ni kwamba ndoa nzuri au mbaya inategemea na malezi au tabia ya mtu kwa ujumla. Ndoa nyingi ambazo mmoja yuko juu sana na mwingine yuko chini sana, mara nyingi huwa ni ya maigizo.
Nje wanaonekana wana ndoa, ndani ni shida. Binafsi sijaweza kufanikiwa kushuhudia ndoa nyingi za wanawake matajiri sana au wenye majina makubwa ambazo ndani zina amani sana, labda kama watakuwa imara katika dini.

Kwa hiyo kama unafikiria kuoana na mwanamke imara sana kiuchumi, au kielimu, sikushauri uache au uendelee, uamuzi ni yako, ila jitahidi kuhoji ni kwanini hajaolewahasa kama ana umri wa miaka 35 na kuendelea.
Najua atakueleza sababu nyingi kwanini aliachana na fulani, ambazo nyingi zitakuwa ni za kuonyesha alioachana nao ndio walikuwa wabaya, ndivyo wengi wanavyofanya.
Tafakari kwa makini zaidi, hasa kama alishawahi kuwa na mtoto au watoto au kuwapo kwenye ndoa na kutalakiana.Kuwa kwenye ndoa ni kuzuri, ni hatari zaidi kama unakuwa kwenye ndoa na mtu ambaye hakupi amani, kwani kitaalam utakufa haraka kwa kupata magonjwa kama ya moyo nk.Heri kuishi mpweke kuliko kuwa kwenye uhusiano usiokupa amani.
TAFAKARI SANA; Kama unaanzisha na mtu ambaye tayari alishakuwa kwenye ndoa, uwe makini mno. Lakini uwe makini zaidi kama mtu huyo naye wazazi wake wametalakiana, uwezekano wa ndoa yenu kutofika mbali ni mkubwa, kwa sababu katika fikra za mtu huyo huwa wanapata majibu ya haraka achana na mimi bwana mbona hata baba aliachana na mama na aliishi.
KWA WANAOTAKA KUANZISHA UHUSIANO; Pata muda wa kumchunguza vizuri mwenzi wako kabla ya kuamua awe mke au mumeo. Pia ni vizuri kutofanya ngono, kwa sababu hilo tendo ndilo linalosababisha wanawake wengi wanaishia kudanganywa.eeeh unakuta mtu hamjakubaliana kuoana halafu mko kwenye tendo unamuuliza unajisikiaje.eeeeh kwa hiyo utanioa? Haaa ha ha!! Nafikiri unachotafutwa hapa ni kudanganywa.
Utakachojibiwa ni kwamba Unataka ndoa, haina shida nitakuoa, hata kesho.eeeh ni kwa sababu jamaa wakati huo akili yake inakuwa haiko hapo, kinachoongea ni mdomo, lakini yeye hayuko. Kwa hiyo ndugu zangu wadada, lazima uangalie unaongea naye mtu wakati gani.
ZAWADI GANI NZURI KWA MWENZI WAKO?; Kuna baadhi ya wasomaji wameuliza je ni zawadi gani nzuri ya kumpa mwenzi wako?
Hili swali naona kama tunateganamaana ukweli watu siku hizi wanapenda fedha zaidisawa unaweza kumpelekea ua, unaweza kununua nguo nk, lakini watu wanapenda fedha.
Zawadi ifaayo katika maisha ya ndoa ni kupendana kwa dhati na kufanyiana mambo mazuri. Mheshimu mwenzi wako, na endelea kubuni mambo mazuri ya kumfanyia. Kama kweli unampenda, ni wazi hutapenda awe mnyonge. Katika mapenzi kila mwanandoa anapaswa kufahamu kuwa analo deni la kumpenda na kumfanyia mema mwanandoa mwenzake.
MADA NA DISMAS LYASSA WA MWANASPOT
No comments:
Post a Comment