WADAU mbalimbali leo watashuhudia uzinduzi wa shindano la
Redd’s Miss Tanzania 2013 linalotarajiwa kuzinduliwa leo na
kushirikisha watu mbalimbali.
Akizungumza jana, Ofisa Habari
wa Kamati ya Miss Tanzania, Hidan Rico, alisema kila kitu kiko tayari
kwa uzinduzi huo uliopangwa kufanyika ukumbi wa Serena jijini.
Rico alisema kuwa, uzinduzi huo ulioandaliwa na wadhamini wakuu wa
shindano hilo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha
Redd’s, unatarajiwa kuwakutanisha wapenzi wa urembo na wadau
mbalimbali, wakiwamo mawakala wanaoandaa mashindano ya kumsaka Redd’s
Miss Tanzania katika hatua za awali, kanda, mikoa hadi taifa.
Aidha, Redd’s Miss Tanzania, Brigite Alfred, naye atakuwepo sambamba
na warembo wengine walioshika nafasi za juu katika shindano la taifa.
“Baada ya uzinduzi huo, mawakala wote wataanza mchakato wa kuandaa
mashindano katika ngazi za wilaya, mikoa, kanda na baadaye taifa,”
alisema Rico.
No comments:
Post a Comment