EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, March 5, 2013

TANESCO hoi...Yakusanya bilioni 2.3/- kwa siku, yatumia bilioni 5.4/-

SHIRIKA la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO) limekana kuwepo mgawo wa umeme kwa sasa huku likikiri kuwa hali ya upatikanaji wa nishati hiyo iko katika dharura na haijarejea katika hali ya kawaida kama inavyotakiwa.
Ufafanuzi huu unakuja baada ya gazeti hili kuripoti hali tete ya kifedha inayolikabili shirika hili na hivyo kutishia taifa kuingia gizani wakati wowote.
Hata hivyo TANESCO na serikali kupitia kwa Wizara ya Nishati na Madini wamekuwa kimya kwa muda pasipo kuzungumzia mgawo wa umeme ambao umekuwepo kwa wiki takriban mbili katika maeneo mengi nchini.
Akizungumza jana makao makuu ya shirika hilo Ubungo, jijini Dar es Salaam, Kaimu 

Mkurugenzi Mkuu, Felchesmi Mramba, alisema kuwa hakuna mgawo wa umeme kwa sasa na kwamba ikitokea serikali ingetangaza.
Pamoja na kukanusha kuwepo kwa mgawo, Mramba alisema ukweli ni kwamba bado nchi iko katika hali ya dharura na hali ya umeme haijarejea katika hali yake ya kawaida kiasi cha kuondoka katika hali ya dharura.

“Ushahidi wa kwamba bado tuko katika hali ya dharura ni kwamba bado mitambo ya dharura tuliyokodi kupambana na hali ya umeme inaendelea kuhitajika lakini pia mabwawa hayana maji ya kutosha kukidhi mahitaji ya umeme bila kuhitaji mitambo ya matufa,” alisema.
Aliongeza kuwa vilevile miundombinu ya gesi haiwapi gesi ya kutosha kuwasha mitambo yote ya gesi ya megawati 501.
Mramba alibainisha kuwa tangu Julai mwaka 2012 hadi Februari 2013, serikali imetumia jumla ya sh bilioni 231.2 kama ruzuku kwa TANESCO kwa ajili ya kununua mafuta ya mitambo.

“TANESCO kutoka kwenye mapato yake imetumia jumla ya sh bilioni 423.3 katika kipindi hicho kununulia mafuta, hivyo fedha yote iliyotumika kununulia mafuta ndani ya kipindi hicho ni sh bilioni 654.5,” alisema.
Mramba aliongeza kuwa mitambo ya dharura inahitaji fedha nyingi kuiendesha kulinganisha na bei halisi ya kuuza umeme huo. Akitolea mfano alisema kuwa ili kuzalisha zinahitajika megawati 365 kwa mafuta (Dizeli-lita 1,368,00, HFO-LITA 500,000 na Jet A1-Lita 518,000 kwa siku.
Alisema kuwa jumla ya sh bilioni 5.4 zinahitajika kila siku au sawa na sh bilioni 162 kwa mwezi na kwamba mapato yanayotokana na kuuza asilimia 100 ya umeme wote unaozalishwa ni sh bilioni kwa siku sawa na takriban sh bilioni 70.2 kwa mwezi baada ya kuondoa kodi na tozo mbalimbali.

“Hata kama TANESCO ingeamua isilipe mishahara wala isifanye matengenezo ya mitambo, isinunue vifaa vya kuunganishia wateja, au isiingie gharama nyingine zozote, bado ingepata hasara ya karibu sh bilioni 90 kila mwezi,” alisema.
Mramba aliongeza kuwa kwa sababu kuna matumizi mengine muhimu ya kiuendeshaji, TANESCO inajikuta ikipata hasara kubwa zaidi kwa mwezi.
Kuhusu deni la Songas, mkurugenzi huyo alikiri kuwa ni kweli kampuni hiyo inaidai TANESCO na akasisitiza kuwa mkataba kati ya Songas na TANESCO unaruhusu hali hiyo.
Hata hivyo, kauli hiyo inatofautiana na kauli ya Naibu Waziri wa Nishari na Madini, George Simbachawene, aliyesema jana asubuhi kuwa wanaoshinikiza kuwa kuna deni kati ya Songas na TANESCO ni madalali tu.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate