GENGE la wahuni katika Kituo cha Mabasi Mbezi Louis, wilayani
Kinondoni, Dar es Salaam limeonekana kushindikana kudhibitiwa kutokana
na genge hilo kuendelea kujikusanyia fedha kutoka kwa madereva kwa
nguvu.
Akizungumza mmoja wa madereva, Salehe Juma,
alisema walijaribu kutoa taarifa Kituo cha Polisi Kimara, lakini hakuna
hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kudhibiti hali hiyo.
Alisema kituo hicho hivi sasa hakina usalama kutokana na usumbufu
wanaofanyiwa madereva na genge hilo kwa kuwalazimisha kila wanapoingia
kituoni hapo kuwatoza fedha.
“Hiace hutozwa sh 1,500 na Coaster sh 2,000 tena bila ya kupewa stakabadhi.
Huu ni unyang’anyi wa wazi kabisa.
Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, wakati anakifungua kituo hiki alisema
ni marufuku magari yote yanayoingia pale kutozwa ushuru wa aina yoyote
pia hapatakiwi kuendeshwa biashara yoyote ile,” alisema Juma.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Msemaji wa Wizara ya Ujenzi, Martin
Ntemo, alisema wahusika wakuu ni Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri na Nchi
Kavu na Majini (Sumatra).
Hata hivyo, Meneja wa Sumatra, David Mziray, alisema hilo la kudhibiti
vitendo hivyo haliko kwao bali wahusika ni halmashauri, kwa kuwa vituo
hivyo viko chini yao.
Naye Msemaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Sebastian
Mhowela, alisema kituo hicho kinamilikiwa na Wakala wa Barabara
(TANROADS), lakini hata hivyo kuna ulazima wa kuwakamatwa matapeli hao.
No comments:
Post a Comment