Ukiachilia mbali mastaa hawa, wako wengine wanaokuja juu kwa sasa
ambao watakuja kuchukua nafasi zao kina Omotola kama wao walivyochukua
vijiti kwa kina Liz Benson.
Sura hizi mpya sio tu ni vijana bali wana sifa lukuki kama ilivyo kwa mastaa wenzao waliotangulia.

Kwanza wanavutia na pia wana vipaji.
Miongoni mwao wameshinda mataji kadhaa yakiwamo ya urembo na hata
uanamitindo.
Je, ungependa kuwafahamu? Hii hapa ni orodha ya waigizaji chipukizi wanaosumbua katika fani ya filamu Nollywood. Licha ya kuwa na msururu mkubwa lakini hawa ndio gumzo kwa sasa;
ABUJA, NIGERIA

KAMA ilivyo kwenye soka, katika filamu pia huwa kuna vizazi na vizazi. Kwa kawaida kila kizazi huwa na nyota wake. Na hivi ndivyo ilivyo kwa tasnia ya filamu nchini Nigeria.
Wako waliowahi kuwika na kufanikiwa kuliweka juu jina la Nigeria.
Miongoni mwao ni pamoja na wakongwe kama vile Patience Ozukwu, Liz
Benson, Regina Askia, Clarion Chukwura na Hilda Dokubo
Licha ya kuwa juu kwa wakati huo ni ukweli usiopingika kuwa bado wanaendelea kufanya vizuri kwa sasa.
Katika kizazi kilichopo wapo mastaa wa kike ambao wanatamba zaidi. Unapoweka orodha ya mastaa hao huwezi kukosa watu kama Omotola, Genevieve, Mercy Johnson, Chika Ika, Stella Damasus, Ini Edo na Tonto Dike.

Damilola Adegbite
Damilola Adegbite hana muda mrefu kwenye filamu. Lakini kwa jinsi anavyofanya kazi kwa bidii anakubalika na wapenzi wengi wa filamu za Kinigeria.
Hivi sasa anakuja na filamu yake mpya iliyotengenezwa na prodyuza, Michelle Bello itakayofahamika kwa jina la Flower Girl.

Kwa jinsi alivyoitendea haki filamu hiyo hutasita kumuita Flower.
Licha ya filamu hiyo, mrembo huyu aliwahi kutokea kwenye tamthilia moja
maarufu nchini Nigeria inayofahamika kwa jina la Tinsel akiigiza kama
Thelma Duke. Hapo ndipo alipoamua kutoka huko na kujikita kwenye filamu.
Lilian Esoro
Lilian Esoro
Naye alianzia kwenye tamthilia. Aliwahi kufanya tamthilia ya Clinic Matters akiigiza kama Nurse Abigail
Kutokana na juhudi aliyokuwa nayo katika suala zima la uigizaji,
hivi karibuni ameungana na wakali Mercy Johnson na Funke Akindele kwenye
kinyanganyiro cha tuzo za Africa Magic Viewers Choice (AMVCA), yumo
katika kipengele cha Mwigizaji Bora wa kike katika kifungu cha
uchekeshaji.
Beverly Naya
Beverly Naya
Ni miongoni mwa warembo wenye kujiamini. Hii ni kutokana uwezo
alionao katika suala zima la uigizaji. Mwaka jana aliingia katika
kinyanganyiro cha kuwania nafasi ya mwigizaji bora katika mitindo
kupitia jarida la FAB nafasi ambayo ilienda kwa Rita Dominic baada ya
kuwabwaga waigizaji wengine kama Genevieve Nnaji, Omotola Jalade na Nse
Itse-Akpan.
Ukiachilia mbali kushiriki mrembo huyu ameshawahi kushinda tuzo
kadhaa. Miongoni mwa tuzo ni pamoja na ile ya Kipaji Chipukizi Bora kwa
mwaka 2010. Ilikuwa kwenye tuzo za ubora za Nollwood, pia mwaka 2011
aliwahi kushinda tuzo ya Msanii anayekuwa kwa kasi.
Biola Ige
Biola Ige
Biola Ige sio mgeni sana kwenye fani ya uigizaji. Ispokuwa kutokana
na kuzongwa na shughuli za utafutaji maisha alitoka kidogo. Lakini kwa
sasa amerudi tena katika tasnia ya uigizaji.
Wapenzi wa filamu wanamtaja kuwa ni miongoni mwa waigizaji wenye
macho mazuri katika Nollywood, si hivyo tu anatajwa pia kuwa mwenye umbo
la kuvutia.
Katika kipindi cha miaka minne alichodumu kwenye tasnia ya uigizaji, ameripotiwa kuigiza filamu 20.
Collete Orji
Collete ameingia kwenye tasnia ya uigizaji muda mfupi uliopita. Lakini kutokana na umahiri wake katika uigizaji, tayari ameweza kukubalika hata kwa watengenezaji filamu mbalimbali.
Ni miongoni mwa warembo waliojaaliwa uzuri , kipaji na hata umbo la kuvutia. Kutokana na sifa zake hizo ameweza kupata nafasi katika filamu kadhaa zikiwamoStrength of a Woman, Blue Blood, Raindrop na Two Can Play That Game.
Angel Ufuoma
Kitaaluma Angel Ufuoma ni Mwanasheria. Lakini baada ya kugundua ana kipaji cha ziada ambacho ni uigizaji hakusita kujiingiza huko.
Amekuwa kwenye fani ya filamu kwa muda wa miaka mitatu sasa. Lakini amekuwa akiigiza kwa umahiri mkubwa sana kiasi cha kukubaliwa na wengi.
Chelsea Eze
Sifa yake ya kushinda tuzo kadhaa za vipaji, ilitosha kumweka juu kwenye tasnia ya filamu na hata kuwa miongoni mwa waigizaji wa kike wanaokuja juu kwa sasa.
Namzungumzia mrembo aliyeigiza katika filamu za Two Brides And A Baby, Twist,Timeless Passions na Hood Rush.
Kutokana na umahiri wake, waongozaji na hatawaigizaji wakubwa wamekuwa wakimkubali na hivyo kuigiza naye kwa kuwa mwigizaji msaidizi na hata mwigizaji mkuu. Kujituma kwake ndio siri ya mafanikio yake.
Tope Osoba
Kama ilivyo kwa waigizaji kama Omotola Jelade au Mercy Johnson, mwigizaji huyu ana uwezo mkubwa wa kushika nafasi mbalimbali tena, yaani uhusika wowote.
Katika kudhihirisha hilo hakusita kufanya maajabu katika filamu za Gucci Girls, Omo Tee, Oogun Mi, 21 Million.
Urembo na kipaji alichonacho vimekuwa vikimwongezea mapenzi dhidi ya mashabiki wake na hivyo kuzidi kuonekana tishio katika tasnia ya uigizaji.

No comments:
Post a Comment