BABA wa marehemu Steven Kanumba, mzee Charles Kanumba amefunguka kuwa
haoni ulazima wa kuliona kaburi la mwanaye na kuhusu kufanya maombi
mwaka mmoja baada ya kifo, alifanya akiwa huko nyumbani kwake Shinyanga.
Akizungumza
na Ijumaa kwa njia ya simu hivi karibuni, mzee Charles alisema mtu
anapofariki kikubwa ni kuombewa na hilo la kwenda kulitazama kaburi lake
haliwezi kuwa na faida.
“Mimi nilifanya sala ya kumuombea Kanumba
pamoja na mtoto wa dada yake ambaye walikufa kwa kufuatana kwenye Kanisa
la AIC Shinyanga,” alisema mzee huyo na kuongeza;
“Mtu akishakufa
kinachobaki ni kumuombea huko aliko na kaa ukijua kwamba huku ndiyo
kwenye chimbuko la marehemu hivyo nisingeweza kwenda kufanyia maombi
kwenye mji mwingine.”
No comments:
Post a Comment