Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amesema watakata rufaa kwa
kamati ya maadili kwa kuwa adhabu aliyoitoa Spika Anne Makinda kwa
wabunge watano wa Chadema hakuzingatia kanuni na taratibu za Bunge.
Mbowe amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua ya Spika Makinda kubariki adhabu iliyotolewa Aprili 17, mwaka huu na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Msemaji huyo wa kambi ya upinzani Bungeni, amesema Spika Ndugai alikiuka baadhi ya taratibu wakati wa kutoa adhabu.
Mbowe
amesema pamaja na Wabunge wa chama chake kupewa adhabu hiyo wabunge wa
upinzani wataendelea kuhoji na kusimama bungeni pale watakapoona mambo
hayaendi kama taratibu za Bunge zinavyoelekeza.Mbowe amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua ya Spika Makinda kubariki adhabu iliyotolewa Aprili 17, mwaka huu na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Msemaji huyo wa kambi ya upinzani Bungeni, amesema Spika Ndugai alikiuka baadhi ya taratibu wakati wa kutoa adhabu.
Pia amesema wataendelea na msimamo wao kwa kuwa Chadema na wako kwa ajili ya maslahi ya wananchi waliowachangua.
Wabunge wa Chadema waliopewa adhabu hiyo ni Highness Kiwia (Ilemela), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Godbless Lema (Arusha Mjini), Hezekiah Wenje (Nyamagana), na Peter Msigwa (Iringa Mjini).
No comments:
Post a Comment