LISEMWALO lipo, kama halipo lipo njiani laja… Rihanna anavumishwa kuwa na ujauzito wa Chris Brown.
Uvumi
huo ulioripotiwa na mitandao kibao ya habari ya Marekani, umekuja baada
ya supastaa huyo wa muziki wa pop kufuta shoo nne za ziara yake ya
Diamond World Tour iliyoanza Machi 8 akilalamika kuwa “mgonjwa”.
Kama
kuna ukweli kuhusu uvumi huo, hakutakuwa na mshangao mkubwa kwa
mashabiki wake, kwani Desemba mwaka jana alisema kuwa anataka mtoto
baada ya kurudiana tena na Chris.
Rihanna
mwenye miaka 25, alionekana akitoka kwenye jengo la matibabu la Beverly
Hills jijini Los Angeles Jumanne iliyopita, na wadadisi wanaamini kuwa
ziara yake hiyo kwa daktari haina uhusiano na tatizo la koo linaloelezwa
kumuweka nje ya steji.
Lakini chanzo cha karibu na mkali huyo anayetamba na kibao chake ‘Diamond’ kimeiambia Gossip Cop kuwa hatarajii kupata mtoto.
Mtu
mwingine wa ndani ameuambia mtandao wa HollywoodLife.com kwamba Rihanna
“ni mgonjwa tu”, na akaongeza, “sorry, si wakati huu. Yeye si
mjamzito!”
No comments:
Post a Comment