UONGOZI wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umesema usafiri wa
treni jijini Dar es Salaam utaanza tena leo baada ya kusitishwa kwa muda
kutokana na kuharibika kwa miundombonu.
Usafiri huo ulisitishwa kwa wiki tatu kuanzia Machi 24 mwaka huu
kutokana na kuharibika kwa miundombinu kulikosababishwa na mvua.
Taarifa iliyotolewa na Ofisa Uhusiano wa shirika hilo, Midladjy Maez,
kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini,Kipallo Kisamfu,
ilieleza kuanza tena kwa usafiri huo kunatokana na kukamilika kwa kazi
ya ukarabati wa tuta lililoharibika eneo la Tabata Relini na Mwananchi.
“Wahandisi wa Kampuni Hodhi za Mali na Uendelezaji wa Miundombinu ya
Reli (Rahco) walikabidhi eneo hilo kwa wahandisi wa TRL Aprili 19 mwaka
huu.
“Pamoja na ukarabari huo kukamilika, ukarabati wa kuimarisha eneo hilo
utaendelea kufanywa na Rahco,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
taarifa hiyo ilieleza kuwa hakuna mabadiliko ya nauli na kwamba kila
abiria mtu mzima atatakiwa kulipia sh 400 na watoto na wanafunzi sh 100
kwa safari moja.
No comments:
Post a Comment