Mabrouk alitoa kauli hiyo alipozungumza na kituo kimoja cha redio
jijini Dar es Salaam jana na kuongeza kuwa wanaolalamika ni wale
walioingia jijini huku wakiwa hawana shughuli maalumu za kufanya.
Alisema ugumu wa maisha haukusababishwa na kupanda kwa nauli bali
ulikuwepo tangu utawala wa awamu ya kwanza na utaendelea kuwepo katika
tawala mbalimbali zijazo.
“Kwa watu tulioishi pamoja katika maisha ya ugumu ugumu nikisema hivyo
wananielewa, lakini najua wapo walionufaika kutokana na kuwa na jamaa
ambao walikuwa viongozi katika serikali; hao labda ndio wanaweza
kushindwa kujua ugumu wa maisha katika nchi hii.
“Pia wananchi wajue kila kitu kizuri kina gharama zake, hivyo ili
kuboresha huduma zetu za usafiri ni lazima wananchi wakubali kuchangia
kile kinachostahili,” alisema Mabrouk.
Akizungumzia mfumo wa huduma ya usafirishaji jijini kuwa wa kampuni,
Mabrouk alisema haukwepiki bali ni muhimu kwa wamiliki wa daladala
kutumia fursa hiyo kujiunga na kuanzisha kampuni.
No comments:
Post a Comment