Katika harakati za kusaka wenzi wa maisha, vijana wengi wamekuwa
wakibabaika juu ya sifa za mwenzi ambaye anaweza kuwa sahihi katika
maisha yake. Hili limekuwa tatizo sugu sana kwa vijana wengi!
Lakini vijana wa sasa huhadaika zaidi na mvuto wa sura na maumbile ya mtu wakifanya kama kipimo kikuu cha anayefaa kuwa mwenzi wa maisha, jambo ambalo ni makosa makubwa sana. Mvuto si kipimo cha mwenzi anayefaa kuingia kwenye ndoa.
Kudanganyika na uzuri wa nje pekee siyo kati ya sifa muhimu zaidi za kumfanya awe na vigezo vya kuwa mwenzi wako wa maisha. Zamani, wazee wetu walikuwa wanatizama kwanza heshima na uchapakazi kama vipimo vya awali kabisa vya kumpa sifa mwanamke kuolewa.
Siku hizi ni kunyume chake! Lakini inashauriwa kuwa makini sana na uchaguzi wako wa mke/mume kwani kufanya maamuzi yasiyo sahihi ni sawa na kujirudisha mwenyewe nyuma. Kuwa na msimamo, fanya uchaguzi ulio sahihi, ambao hautakufanya baadaye ujutie!
Ndoa ni agano, hivyo ni vyema ukawa umejihakikishia kwamba hujafanya makosa kabisa katika uchaguzi wako. Vipo vigezo muhimu zaidi, ambavyo unatakiwa kuviangalia kwa mwanamke ambaye unataka awe mkeo. Hebu tuanze kuviona.
JIULIZE, UNAMPENDA?
Kitu cha kwanza kabisa ambacho unatakiwa kuhakikisha unakifikiria ni juu ya mapenzi yako kwake! Sema na moyo wako ukupe ukweli juu ya hilo, usikurupukie mapenzi, usije ukamuona msichana siku moja amevaa suruali inambana kiasi cha kuonyesha umbile lake halafu ukamtamani ukadhani unampenda, utakuwa unapotoka!
Mapenzi ya kweli huanzia moyoni, jiridhishe kwanza ndipo ukubali kumwingiza katika moyo wako. Kumbuka kuwa unapoamua kufunga ndoa na mtu ni ahadi ambayo mmeahidiana mbinguni na duniani, ni ahadi ambayo inapaswa kutenganishwa na kifo tu, sio vinginevyo!
CHUNGUZA, ANAKUPENDA?
Jambo la pili ambalo unatakiwa kuliangalia ni kuhusu mapenzi yake ya kweli kwako. Wataalam wa Mambo ya Mapenzi wanasema, ingawa ni vizuri kuishi na mtu unayempenda lakini pia ni lazima awe anakupenda! Siyo vigumu sana kumfahamu mwenzi anayekupenda, lakini pia inawezekana ukaona anakupenda kumbe ni danganya toto!
Kimsingi katika hili ni lazima utumie akili yako yote
uweze kutambua hilo. Katika makala zangu zilizopita nilianisha sifa za
mpenzi mwenye mapenzi ya dhati, lakini kwa kuongezea ni kwamba,
anayekupenda huwa mvumilivu, anayekusikiliza pia mwenye kuwajali ndugu,
marafiki na jamaa zako, anayekuheshimu na kutambua thamani yako. Lakini vijana wa sasa huhadaika zaidi na mvuto wa sura na maumbile ya mtu wakifanya kama kipimo kikuu cha anayefaa kuwa mwenzi wa maisha, jambo ambalo ni makosa makubwa sana. Mvuto si kipimo cha mwenzi anayefaa kuingia kwenye ndoa.
Kudanganyika na uzuri wa nje pekee siyo kati ya sifa muhimu zaidi za kumfanya awe na vigezo vya kuwa mwenzi wako wa maisha. Zamani, wazee wetu walikuwa wanatizama kwanza heshima na uchapakazi kama vipimo vya awali kabisa vya kumpa sifa mwanamke kuolewa.
Siku hizi ni kunyume chake! Lakini inashauriwa kuwa makini sana na uchaguzi wako wa mke/mume kwani kufanya maamuzi yasiyo sahihi ni sawa na kujirudisha mwenyewe nyuma. Kuwa na msimamo, fanya uchaguzi ulio sahihi, ambao hautakufanya baadaye ujutie!
Ndoa ni agano, hivyo ni vyema ukawa umejihakikishia kwamba hujafanya makosa kabisa katika uchaguzi wako. Vipo vigezo muhimu zaidi, ambavyo unatakiwa kuviangalia kwa mwanamke ambaye unataka awe mkeo. Hebu tuanze kuviona.
JIULIZE, UNAMPENDA?
Kitu cha kwanza kabisa ambacho unatakiwa kuhakikisha unakifikiria ni juu ya mapenzi yako kwake! Sema na moyo wako ukupe ukweli juu ya hilo, usikurupukie mapenzi, usije ukamuona msichana siku moja amevaa suruali inambana kiasi cha kuonyesha umbile lake halafu ukamtamani ukadhani unampenda, utakuwa unapotoka!
Mapenzi ya kweli huanzia moyoni, jiridhishe kwanza ndipo ukubali kumwingiza katika moyo wako. Kumbuka kuwa unapoamua kufunga ndoa na mtu ni ahadi ambayo mmeahidiana mbinguni na duniani, ni ahadi ambayo inapaswa kutenganishwa na kifo tu, sio vinginevyo!
CHUNGUZA, ANAKUPENDA?
Jambo la pili ambalo unatakiwa kuliangalia ni kuhusu mapenzi yake ya kweli kwako. Wataalam wa Mambo ya Mapenzi wanasema, ingawa ni vizuri kuishi na mtu unayempenda lakini pia ni lazima awe anakupenda! Siyo vigumu sana kumfahamu mwenzi anayekupenda, lakini pia inawezekana ukaona anakupenda kumbe ni danganya toto!
Mwanamke anatakiwa kujitoa kwako kikwelikweli na hapo ndipo utakapoingia kwenye ndoa yenye amani na furaha. Mwanamke anayetakiwa kuwa na wewe katika maisha ya ndoa ni lazima moyo wake uwe umejiachia kwako sawasawa.
ANA SIFA ULIZOTARAJIA?
Linaweza kuwa swali tata kwako, lakini kamwe lisikuchanganye akili yako, hapa unatakiwa kujiuliza juu ya uliyotarajia kwake, ni kweli unayapata yote? Hapa kuna vipengele viwili ndani ya hiki kimoja. Kwanza kabla ya uhusiano na pili, ndani ya uhusiano.
Nikianza na kabla ya uhusiano, hapa namaanisha kwamba, ana sifa zote ambazo ulikuwa unatarajia kwa mpenzi wako ajaye, ambaye ndiye huyo unayetarajia kuingia katika uhusiano naye. Ni kweli ana kila kitu kinachokuvutia kiasi kwamba hutathubutu kumsaliti?
Ukishajiridhisha na hilo, unaweza kuingia katika uhusiano lakini siyo kwa kasi kubwa, hapa namaanisha kwamba, unaingia katika kipindi cha urafiki ambacho huweki kila kitu wazi, hivyo katika kipindi hiki utaweza kujua kama unapata kile ulichotarajia.
Chunguza tabia zake kwa makini katika kipindi hiki, toka naye katika matembezi ya pamoja, huku ukiwa umemweka katika kipimo ambacho hata yeye mwenyewe atakuwa hafahamu. Lazima mwisho wa siku utaweza kugundua kwamba, chaguo lako lilikuwa sahihi au lah.
ANAJALI?
Hata kama ni mzuri kiasi gani, ana mvuto kiasi gani, anakubalika na marafiki zako kiasi gani, lakini vyote hivyo vinaweza kupoteza maana kama hataonyesha anavyojali thamani yako wewe kama mpenzi wake.
Ninapozungumzia kujali, nakuwa nimekwenda mbali zaidi, anavyojali familia yako, marafiki zako na hata wewe mwenyewe. Hutakiwi kuwa na mwanamke ambaye akili yake haiwazi chochote juu ya maisha. Mwanamke anapaswa kuwa makini, akili ziwe zinafanya kazi sawasawa na awe na mchango mkubwa wa mawazo kwenye familia.
MNYENYEKEVU
Sifa ya mvuto wake, inaweza kuharibiwa na kukosa uchangamfu na unyenyevu. Mwanamke hata kama ni mzuri kwa kiwango gani, akipoteza sifa hizi, uzuri wake ni kama unakuwa umepungua. Uchangamfu huu uanzie kwako, asiwe mwanamke mkimya kupitiliza, hali ambayo inaweza kutafsiriwa kwamba anaringa.
Lakini pia, uchangamfu huu anatakiwa auonyeshe hata kwa rafiki zako pamoja na ndugu zako. Mwanamke mwema ni yule mwenye unyenyekevu kwa mumewe pamoja na ndugu zake.
...Umenipata?
Uzuri wa mwanamke hauna maana ya ubora wa kuwa mke, siyo kila mwanamke anaweza kuwa mke! Mchunguze kwa makini sana mwenzi wako, hakikisha ana sifa nilizozitaja na zingine muhimu zaidi, lakini kubwa kuliko yote, mwanamke huyo lazima awe anakupenda kwa mapenzi ya dhati.
Kama hakupendi mtawezaje kuishi katika ndoa? Naweka kituo kikubwa hapa, nikiwataka tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri zaidi. Nawatakieni week-end njema marafiki zangu.
No comments:
Post a Comment