Ni kauli ya TCRA ikinukuu sheria ya mawasiliano. Lengo ni kudhibiti matumizi mabaya ya simu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA ), Profesa
John Nkoma, akizungumza kwenye mkutano wa pamoja na viongozi wa Kampuni
za Simu kuhusu usajili wa laini za simu Dar es Salaam jana.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kisheria mtu anayetumia simu isiyosajiliwa akikamatwa anaweza kutozwa faini ya Sh500,000 au kwenda jela miezi sita.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kisheria mtu anayetumia simu isiyosajiliwa akikamatwa anaweza kutozwa faini ya Sh500,000 au kwenda jela miezi sita.
‘‘Kwa mujibu wa kifungu cha 131 cha sheria ya mawasiliano mteja au muuzaji wa namba ya simu ambayo haijasajiliwa atatozwa faini ya Sh500,000 au kifungo cha miezi mitatui’’ ilielezwa jana.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema hayo alipokutana na wadau wa mawasiliano jijini hapa jana. Profesa Nkoma alisema namba za simu ni lazima zisajiliwe kwa mujibu wa sheria ya mawasiliano ya elekroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010.
Ufafanuzi wa TCRA umekuja baada ya kuwapo malalamiko ya watu wa kada mbalimbali kwamba mawasiliano yao ya simu yanaingiliwa na kuchapishwa katika vyombo vya habari.
Katika maelezo yake ya jana, Pofesa Nkoma alisema
kwa mujibu wa kifungu cha 130 cha sheria ya EPOCA ya mwaka 2010, mtu
ambaye atauza au kutoa namba za simu bila ya kusajiliwa atachukuliwa
hatua za kisheria na adhabu yake ni faini ya Sh3 milioni na kifungo cha
miezi 12.
“Katika vikao vya pamoja vilivyofanyika Aprili 4 na Aprili 11 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na kampuni zinazotoa huduma za simu za mkononi, zimekubaliana juu ya hatua za kumaliza tatizo la usajili wa namba za simu na utaratibu wa kufungia namba zote ambazo hazikusajiliwa,”alisema Profesa Mkoma.
Profesa Nkoma alisema kwa kushirikiana na kampuni
za simu na vyombo vya usalama imeanza kampeni endelevu ili kuwabaini
wanaohusika na uvunjifu wa sheria kwa lengo kuwalinda watumiaji wema,
jamii kwa ujumla kwa ajili ya kuimarisha usalama na kuleta maendeleo na
usawa katika jamii.
Pia alisema mikakati iliyopo ya TCRA simu ambazo hazijasajiliwa hazitafanya kazi, hivyo watu ambao hawajajisajili waanze mchakato huo.
Alisema namba za simu zilizosajiliwa ni asilimia
93 na asilimia 7 hazijasajiliwana kwamba asilimia iliyobaki inatakiwa
kuondoka haraka..
No comments:
Post a Comment