MWIMBAJI wa Muziki wa Injili
mwenye muonekano wa ‘mama mwenye ndoa’, Bahati Lusako Bukuku amefunguka
kuwa amepata mchumba lakini tatizo linabaki kuwa mume wake wa zamani,
Daniel Basila ambaye anasuasua kumpa talaka yake, Amani lina mkoba
mkononi.
Akizungumza na ‘balozi’ wetu jijini Dar juzikati, staa huyo anayetamba na wimbo wake wa Dunia
Akizungumza na ‘balozi’ wetu jijini Dar juzikati, staa huyo anayetamba na wimbo wake wa Dunia
Haina Huruma aliweka ‘pleini’ kwamba
hivi karibuni Mungu amemjalia kupata mchumba ambaye anahofia kumwanika
kwa kuwa anabanwa na kifungo cha ndoa yake ya kwanza aliyofunga na
Basila.
Bahati alisema kuwa kifuatacho inabidi adai talaka yake kwa
nguvu zote hata ikiwezekana kufikishana polisi ili aondokane na kifungo
cha ndoa hiyo na aanze mipango ya ndoa kwa kuwa hataki kumtendea Mungu
dhambi.
Alisema kuwa, mara nyingi amekuwa akimkumbusha mumewe huyo wa
zamani kuhusu talaka lakini amekuwa akimwambia asikonde talaka yake ipo
hivyo avute subira.
Bukuku aliolewa na Daniel na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye alifariki dunia mwaka 2006 kabla staa huyo kutengana na mumewe.
Bukuku aliolewa na Daniel na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye alifariki dunia mwaka 2006 kabla staa huyo kutengana na mumewe.
CHANZO CHA HABARI NI MTANDAO WA GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment