Na Gladness Mallya
MSANII wa filamu Bongo, Deogratius Shija ametoa kali ya mwaka baada
ya kusema anajiandaa kugombea ubunge kwa nia ya kutetea haki za wanyama
kwani hawana mtetezi bungeni.
Akichonga na paparazi wetu, Shija
alisema mwaka 2015 kutokana na kwamba kutakuwepo na katiba mpya
atagombea ubunge kama mgombea binafsi kwa ajili ya kwenda kuwatetea
wanyama hao ambao mpaka leo hakuna anayewatetea.
“Nina mpango wa
kugombea ubunge kwa ajili ya kuwatetea wanyama kama paka, mbwa, ng’ombe,
punda na wengine wengi kwani nimegundua binadamu wanawatesa sana na
hawana mtu wa kuwatetea.
“Wazo hili nililipata mwaka jana
nilipotembelea nchi ya Kenya nikakuta kuna wabunge wa kutetea haki za
wanyama hivyo hapa Tanzania katiba hiyo ikipita naamini na mimi
nitakanyaga bungeni,” alisema Shija.
No comments:
Post a Comment