MTANGAZAJI wa Kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Redio, Loveness
Malinzi ‘Diva’ ameifungukia ndoa yake na staa wa muziki wa Kenya,
Jackson Makini ‘Prezzo’ kuwa haiko mbali kwani hatua waliyofikia ni
nzuri.
Akipiga stori hivi karibuni Diva alisema uhusiano wake na
jamaa huyo hakuna wa kuutibua na anamshangaa msichana anayejitambulisha
kwa jina la Boss lady anayedai ameingiliwa.
“Mimi namshangaa huyu
dada anayeniandama kwenye mtandao toka aliposikia nipo na Prezzo, kwa
kifupi kwa Prezzo nimefika na ndoa muda si mrefu utapita ili tuweze
kuishi kama mke na mume” alisema Diva.
Diva alisema kuonyesha kuwa
anakubalika hata kwenye familia ya Prezzo, aliongea na dada wa msanii
huyo ambaye alimtuliza kwa kumwambia kuwa asisikilize maneno ya watu
kwani yeye ndiye wifi yake wa ukweli.
No comments:
Post a Comment