Dodoma.
Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe ameingia katika msuguano wa chinichini na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Peter Serukamba ambaye alidaiwa kuongeza maneno kwenye hotuba ya kamati yake yaliyokuwa yakimlenga waziri huyo binafsi.
Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe ameingia katika msuguano wa chinichini na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Peter Serukamba ambaye alidaiwa kuongeza maneno kwenye hotuba ya kamati yake yaliyokuwa yakimlenga waziri huyo binafsi.
Kutokana na hali hiyo, hotuba iliyokuwa isomwe na Serukamba kama maoni ya kamati baada ya Dk Mwakyembe kuwasilisha hotuba yake, ilibadilishwa dakika za mwisho na kusainiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Juma Kapuya.
Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo (ambaye aliomba
jina lake lihifadhiwe) alisema waliamua kuunda kamati ndogo ya wabunge
wanne kusahihisha lugha iliyotumika katika kuandaa maoni ya kamati hiyo
kuhusu Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha wa
2013/2014.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, wajumbe waligundua kuwa lugha iliyotumika ililenga kushambulia moja kwa moja Dk Mwakyembe ndani ya Bunge jambo ambalo lilkuwa kinyume cha makubaliano ya kamati.
Hata hivyo, Serukamba akizungumza na gazeti hili alikana kubadili hotuba hiyo na kuongeza kuwa; “Mimi nimerudi jana, kwa kawaida kamati ikishajadili suala la hotuba kuandikwa tunamwachia Katibu na akimaliza anairudisha kwetu wabunge. Hivyo nilichokisoma ndicho tulichokubalina na wajumbe wa kamati hiyo.”
Aliongeza: “Msitake kunigombanisha na mheshimiwa
Waziri, mimi ndiyo kwanza nimeingia asubuhi hii hakuna kilichobadilika
katika hotuba hiyo.”
Gazeti hili lilifanikiwa kuona nakala mbili za hotuba za kamati, moja ikiwa na saini ya Serukamba na nyingine ikiwa imesainiwa na Profesa Kapuya na zote zina tarehe inayofanana ambayo ni Mei 16, 2013.
Kwa upande wake Kapuya katika majibu ya maandishi
kwa gazeti hili alisema si kweli kwamba ziliandikwa hotuba mbili.
“Habari hizo hazina ukweli, kamati yangu ina utaratibu wa kuandaa hotuba
yetu na ikishakamilika tunateua kamati ndogo ambayo inapitia hotuba
hiyo kabla ya kuisoma,”alisisitiza Profesa Kapuya.
Majibu ya Serukamba na Kapuya yanatofautiana na
kauli ya Dk Mwakyembe ambaye aliliambia gazeti hili kwamba pia alipata
taarifa za kuwapo kwa mpango huo kutoka kwa
“watu wanaojua na kuthamini kazi yake.”
“watu wanaojua na kuthamini kazi yake.”
“Siyo kila mtu anaweza kukuchukia huwezi kunyimwa
maneno, watu wenye imani na mimi walikuja kunipa taarifa na wakanipatia
ile aliyokuwa ameandika yeye…. ana bahati sana nilikuwa namsubiri kwa
hamu aisome hiyo hotuba yake nilipanga kumchanachana pale pale
asingeamini,”alisisitiza Dk Mwakyembe.
Alipoulizwa kwa nini anafikiri mwenyekiti huyo ameamua kumfanyia hivyo, Dk Mwakyembe alisema; “Siwezi kujua lakini naamini hizi ni mbio tu za mwaka 2015.”
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema hafahamu
kuhusu suala hilo. “Ninachofahamu ni kwamba Serukamba alikuwa amesafiri
kwenda China na mimi nilimwona siku hiyo akisoma maoni ya kamati yake,
kama kulikuwa na tatizo hilo pengine litakuja baadaye ofisini
kwetu,”alisema Ndugai kwa simu.
Via mwananchi.
Via mwananchi.
No comments:
Post a Comment