IMELDA Joseph (21), ameibuka kinara katika kinyang’anyiro cha
kumsaka Redd’s Miss Serengeti 2013 kilichofanyika mwishoni mwa wiki
kwenye ukumbi wa Giraffe Garden Hotel mjini Mugumu mkoani Mara baada ya
kuwabwaga wenzake wanane.
Kwa ushindi huo, Imelda alizawadiwa sh 300,000 na kupata tiketi ya kushiriki shindano la mkoa.
Nafasi ya pili ilikwenda kwa Mariam Omary (18), aliyeondoka na sh
200,000 huku mshindi wa tatu ni Miriam Joseph akijipoza na sh 100,000.
Akitangaza matokeo hayo, mgeni rasmi mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chandi Marwa, alisema kuwa Miss Serengeti
atawakilisha Wilaya ya Serengeti kumtafuta Redd’s Miss Mara katika
shindano litakalofanyika mwishoni mwa mwezi huu mjini Musoma.
Mratibu wa shindano hilo, Mtatiro Kehengu, alisema kuwa kulikuwa na
warembo 12 waliokuwa wamejisajiri, lakini wengine waliondoka kwenye
kambi kwa sababu mbalimbali.
Shindano hilo liliandaliwa na Shanyangi General Supply na kudhaminiwa
na Anita Motel, WMA-Ikona, Giraffe Garden Hotel, Serengeti Serena Hotel,
Mountain Peak, Setco, Nyanza Bottling na Vedastus Mathayo.
No comments:
Post a Comment