Dodoma.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema anaamini chanzo cha kuchafuliwa kwake na wapinzani ni wadhifa wake.
Akizungumza
na mwandishi wetu Dodoma jana, Kinana alisema anaamini kuwa kama
asingekuwa na wadhifa huo, asingesakamwa kwa tuhuma alizoziita za
uzushi.
Aprili 29, mwaka huu, Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa Wizara ya
Aprili 29, mwaka huu, Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa Wizara ya
Maliasili na Utalii, ambaye pia ni Mbunge wa
Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa alimtuhumu Kinana
kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo na kudai kuwa meli
iliyokuwa chini ya uwakala wa Kampuni Sharaf Shipping inayomilikiwa na
Kinana ilikamatwa huko Vietnam na nyara hizo za Serikali.
“Hivi vitu
havinisumbui. Hapa tatizo ni kuwa Katibu Mkuu wa CCM. ‘I am a senior
officer’ (Ofisa Mwandamizi) sasa katika chama changu kama ningekuwa
nimekaa nyumbani nafanya biashara zangu yasingetokea haya.
“Nataka
kuwaambia tu, waelewe kuwa hawawezi kunitoa katika ajenda yangu ya
msingi. Hii ni sawa na mwanajeshi anayekwenda kupigana vita na adui
halafu akawa na vikundi vidogo vinakushambulia kutoka kila upande
kukutoa katika lengo la msingi... ni lazima mtu ukomae na ili
ufanikiwe,” alisema Kinana.
Alisema Msigwa alikuwa katika Kamati ya
Ardhi na Maliasili ya Bunge tangu mwaka 2010 na ukweli wa mambo hayo
anaujua... “Msigwa anajua kabisa nikiwa kama ‘shipping agent’ (wakala wa
meli), sihusiki na kujua kilichopo ndani ya kontena. Wale wanaopaswa
kujua ni meneja wa bandari, mamlaka ya mapato, walinzi na wakala wa
kupakia na kupakua mizigo, kwa kuwa wao ndiyo wanafanya ukaguzi na
kuweka seal (lakiri) …siyo kazi yetu,” alisema.
Kinana aliongeza kuwa
anamini kuwa CCM ni tishio kwa wapinzani ndiyo maana wameanza kumpiga
madongo kwa lengo la kupambana naye. Alipoulizwa kwa nini hajachukua
hatua za kisheria kama anaona amechafuliwa na kama tuhuma hizo hazina
ukweli? Kinana alijibu kuwa anajua kuna njia tatu za kuchukua kuhusiana
na tatizo hilo lakini bado anazifanyia kazi.
“Kwanza unaweza kujieleza kwenye vyombo vya habari. Pia unaweza kukata rufaa kwa Spika na kesi yako kusikilizwa lakini pia unaweza kwenda mahakamani. Bado natafakari cha kufanya.”
Madai ya Msigwa
“Kwanza unaweza kujieleza kwenye vyombo vya habari. Pia unaweza kukata rufaa kwa Spika na kesi yako kusikilizwa lakini pia unaweza kwenda mahakamani. Bado natafakari cha kufanya.”
Madai ya Msigwa
Mchungaji Msigwa alisema
bungeni kuwa: “Kwa bahati mbaya ni kwamba wahusika wengi ambao wanatajwa
kwa ushahidi ni makada maarufu na wengine ni viongozi waandamizi wa
CCM. Tumeshuhudia watuhumiwa wengine wa ujangili ambao Ikulu imediriki
kuwapatia nafasi kubwa za uongozi wa taifa hili, licha ya kutajwa kwenye
ripoti ya uchunguzi kuhusiana na ujangili.”
Alisema mwaka 2009, meli
ya Kampuni ya Wakala wa Meli ya Sharaf Shipping inayomilikiwa na Kinana
ilikamatwa China ikiwa na makontena yenye nyara za Serikali
ikiyasafirisha kwenda Hong Kong.
“Nyaraka zilizopo Ofisi za Wakala wa Usajili wa Kampuni na Biashara (Brela), zinaonyesha kuwa kampuni hiyo ya Kinana ilisajiliwa Oktoba 2003 na kupewa hati na. 47221.
“Nyaraka zilizopo Ofisi za Wakala wa Usajili wa Kampuni na Biashara (Brela), zinaonyesha kuwa kampuni hiyo ya Kinana ilisajiliwa Oktoba 2003 na kupewa hati na. 47221.
CHANZO NI GAZETI LA MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment