Kibaha.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania,
Rais Jakaya Kikwete amewaaga wapiganaji wa Tanzania wanaokwenda DR Congo
kulinda amani kwa kuwadhibiti waasi wa vikundi mbalimbali kikiwamo cha
M23 walioko Mashariki wa nchi hiyo.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi bendera kiongozi wa batalioni ya wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda
kujiunga na jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
katika sherehe za kuwaaga zilizofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani jana.Picha na Ikulu
Kikwete alimkabidhi bendera
kiongozi wa batalioni ya wapiganaji wa JWTZ wanaokwenda kujiunga na
Jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani nchini humo katika hafla
iliyofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani jana. Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali
Davis Mwamunyange ni miongoni mwa mashuhuda katika hafla hiyo.
“Ninawatakia
kila la kheri kwenye mapambano,” Amiri Jeshi Mkuu alimwambia kiongozi
wa Batalioni ya Wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda nchini humo. Tanzania
inaungana na Afrika Kusini na Malawi kufanya kuwapo kwa kikosi cha
askari 3,100 huku Tanzania ikipeleka askari 850 kwa ajili ya kazi hiyo.
Vikosi
vya awali vya Tanzania vimekwishatangulia nchini humo vikiongozwa na
Jenerali James Mwakibolwa anayeongoza Brigedi hiyo chini ya UN, na
tayari amewasili kwenye Mji wa Goma, ambao ndio Mji Mkuu wa Jimbo la
Kivu ya Kaskazini unaokaliwa na waasi wa M23 tangu Aprili 2012.
Kwa
mujibu wa Mtandao wa Monusco, vikosi vingine vya wapiganaji wa Tanzania
na Afrika Kusini vitawasili wiki ijayo wakati Wanajeshi wa Malawi
haijafahamika tarehe ya wao kuwasili.
Msemaji wa wapiganaji wa M23, Kanali, Vianney Kazarama alikaririwa akisema: “Tuko tayari kwa mapambano, wapiganaji wako kambini Rumangabo, wakifanya mazoezi makali ya kushambulia, kujilinda na mbinu za kukabiliana na adui pamoja na kucheza kung fu.
Msemaji wa wapiganaji wa M23, Kanali, Vianney Kazarama alikaririwa akisema: “Tuko tayari kwa mapambano, wapiganaji wako kambini Rumangabo, wakifanya mazoezi makali ya kushambulia, kujilinda na mbinu za kukabiliana na adui pamoja na kucheza kung fu.
No comments:
Post a Comment