Kibanda amefafanua kuwa, miongoni
mwa mapungufu yaliyopewa kisogo na Tume ya Mabadiliko ya Katiba
inayoongozwa na Jaji mustaafu, Joseph Warioba ni pamoja na vyama vya
siasa kuteka nyara mchakato wa mabadiliko ya katiba, wananchi kukosa
kuelimishwa barabara kuhusu mchakato huo na kukosa kuhusishwa kikamilifu
wadau wa shughuli hiyo ya kuunda katiba mpya.
Hii ni katika hali
ambayo, Chama cha upinzani cha CUF kimesema kupitia mwenyekiti wake
Profesa Ibrahim Haruna Lipumba kwamba, serikali inapanga mkakati wa
kuvuruga mchakato wa kuandaa rasimu ya katiba mpya ili iweze kubakia
madarakani kwa zaidi ya muda wa miaka 5 ulioainishwa na katiba ya sasa.
No comments:
Post a Comment