Hatimae meneja Rafael
Benitez ataondoka Chelsea akiwa na tabasabu baada ya timu yake kubeba
ubingwa wa
Kombe la Europa League kwa kuifunga timu ya Benfica ya Ureno
2-1 usiku wa Jumatano katika uwanja wa Amsterdam, Uholanzi.
Hii ni baada ya Branislav Ivanovic kufunga bao maridadi kwa kichwa wakati wa muda wa ziada wa majeruhi.
Tangu alipoingia Chelsea kama kaimu
mkufunzi Benitez amekuwa na wakati mgumu kwani mashabiki wa Old Trafford
wamekuwa hawampendi.
Lakini baada ya kuifunga Benfica mashabiki hao
hao ambao walikuwa hawampendi Benitez waliishangilia ushindi wa timu yao
kwa vifijo na nderemo huku wakisahau chuki waliokuwa nao kwa kaimu
meneja huyo.
Mwaka jana Chelesea ilishinda Kombe la Klabu bingwa bara Ulaya na mwaka huu wamebeba kombe la Europa League.
Bao lakwanza la Chelsea lilifungwa na
mshambulizi Fernando Torres nao Benfica wakapata lao kupitia mwaju wa
penalti uliofungwa na Oscar Cardozo.
Ushindi wa Chelsea unamfanya Rafael Benitez kuwa
meneja wa nne kushinda kombe la Klabu Bingwa Uropa na la Europa League
zaidi ya mara mmoja.
Wengine amabo wamewahi kushinda kumbe hilo zaidi
ya mara moja ni Giovanni Trapattoni: 1977 (Juventus); 1991 (Inter);
1993 (Juventus) ,Luis Molowny: 1985 & 1986 (Real Madrid) Juande
Ramos: 2006 & 2007 (Sevilla).
No comments:
Post a Comment