KUELEKEA shoo maalumu ya Miaka 13, ya mwanamuziki nguli wa bongo
fleva nchini na kiongozi wa bendi yenye msisimko mkubwa ya ‘Machozi
Band’, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ au Jide’ huenda kwa upande wa
wasanii wa Nyumba ya Vipaji ya THT, Linah Sanga na Barnaba mwaka huu
ukawa mchungu kwao kufuatia kuwepo taarifa za kutimuliwa na uongozi wa
juu.
Kwa mujibu wa vyanzo kutoka kwa mtu wa karibu wa Linah kilieleza kuwa mpaka sasa msanii huyo hana raha na wala hajui ataanza vipi katika harakati zake za kimuziki hasa kufuatia hivi karibuni kukacha shoo ya nguli Lady Jay Dee kwa shinikizo kutoka kwa wakubwa zake. Hata hivyo, Linah inadaiwa uongozi wa juu umekaa kikao na hatua iliyofuatia kwenye kikao hicho ni kuwaondoa kabisa kwani huenda wakatia doa wasanii wenzao ndani ya kundi hilo.

“Juzi Linah, haikuwa kawaida yake maana hata alipopigiwa simu kwa ajilhatua zingine alionekana kuwa na hofu, na wala hakutaka
kusikia ushauri wangu ambao nilikuwa nikimhusia kuwa aachane na mawazo
hayo kwani jambo analoliwaza huenda likaisha na hata maamuzi
yatakayotoka yatakuwa ni kawaida” kilieleza chanzo kutoka kwa mtu
wakaribu wa Linan, ambaye hata hivyo alisema kuwa huenda ukweli wa
jambo ukawa hadharani
.
Hata hivyo taarifa za ndani za uongozi wa THT zilibainisha kuwa
mpango wao wa kuwashughulikia wasanii hao upo pale pale na taratibu
zinafuata ilizisilete madhara kwa wasanii waliopo ndani ya THT na watu
wa karibu wanaoiunga THT.
“Wewe nani kakwambia kama tumewaadhibu Lina na Barnaba?, ndio kwanza tunakusikia wewe hizo taarifa, sisi tunafanya mambo yetu wao waache wafanye yao tukiwa nao sie na tunaouwezo wa kuwatimua ilikulinda hadhi ya THT” Kilieleza chanzo hicho ambacho hata hivyo kutokana na usalama wa jina lake tumelihifadhi. Ambapo namba yake inaishia na**08.Aidha, katika ‘ku-balance’ uhondo kamili wa habari hizi wasanii hao wote walipotafutwa kwenye simu zao za mkononi lakini hawakuweza kuwa hewani kwa muda mrefu.. na hata alipopigiwa mtu wao huyo wa karibu naye alizima simu.
Katika kile kinachoeleza kupamba moto shoo hiyo, na kujaa kwa taarifa mbalimbali juu ya wasanii watakaopamba shoo ya miaka 13, Mei 31 ndani ya Nyumbani Lounge, Tayari tiketi zimeanza kuuzwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Saalam.

Shoo hiyo ya kijanja Nyumbani Lounge, patakuwa hapatoshi pale wadau
wa burudani na wastaarabu wote watakapojumuika kwa pamoja ku-shoo love
kwa Lady Jay Dee na Machozi Band, huku listi ya mastaa mbalimbali
wanatarajia kuudhuria sambamba na ‘surprise’ kutoka kwa mastaa hao ambao
kwa sasa wengi wapo kimya wakihofia kutengwa na wazee wa ‘fitina bin
Logiki’.
Awali kulikuwapo na taarifa za kuwapo kwa msanii Matonya, ambaye hata hivyo mtandao wa Lady Jay Dee ulitoa hadharani kuwa mwanamuziki huyo ameshachukua ‘advance’ ya shoo hiyo na wazee wa ‘kuingilia logik’ wameshamtisha Matonya ili ajitoe, lakini akiwa ameshatafuna pesa ya watu.
Mtandao huo wa kijamii blog, ilinukuu kila kitu juu ya Makubaliano baina ya Capt.Gadna G Habashi na Matonya ambapo pia unaweza kuyasoma kupitia (Ladyjaydee.blogspot.com) Pia ulitoa kwa mara ya kwanza picha,maelezo muhimu na video ya wanamuziki hao wawili Linah na Barnaba wakiingia mkataba wa shoo hiyo na pia kuhamasisha watu kufika Mei 13..

No comments:
Post a Comment