Na Erick Evarist
WAKATI nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa Uingereza kwa ziara ya kimuziki, mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ na mkwewe mtarajiwa, Penny wameangusha bonge la sherehe katika Hoteli ya Serena, Posta jijini Dar.

Habari za kuaminika zilizotua kwa paparazi wetu zilidai kwamba,
Jumamosi iliyopita Penny ambaye ni DJ wa Runinga ya DTV alikuwa
akitimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa hivyo akawa amejipanga kufanya
sherehe yake ndogo ya kuzaliwa huku mama wa msanii huyo akiwa naye
amejipanga na dada yake Diamond, Esma ‘Kardashian’ kumfanyia sherehe
mtangazaji huyo.
Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina kilidia
kuwa, Penny alipania kweli kufanya sherehe hiyo na ubavu wake Diamond
lakini mambo yakawa ndivyo sivyo baada ya jamaa kupata shoo hiyo pande
za Uingereza.
“Penny ametimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa sasa alipenda
kufanya pati hiyo na Diamond sema bahati mbaya jamaa yupo Uingereza kwa
hiyo akaamua kufanya na familia ya staa huyo ili kujiliwaza,” kilisema
chanzo makini na kuongeza:
“Penny alijiandaa kwa upande wake, mama Diamond naye na dada Esma wakajiandaa hivyo wakaungana pamoja na kuangusha bonge la sherehe lililohudhuriwa na watu mbalimbali baadhi yao wakiwa ni mastaa.”
“Penny alijiandaa kwa upande wake, mama Diamond naye na dada Esma wakajiandaa hivyo wakaungana pamoja na kuangusha bonge la sherehe lililohudhuriwa na watu mbalimbali baadhi yao wakiwa ni mastaa.”
Picha ambazo Ijumaa imezinasa zinaonesha pati
hiyo ilifana kwa misosi, vinyaji vya kufa mtu ambapo wageni waalikwa
walikula hadi kusaza na kila mmoja aliwapongeza waandaaji wa sherehe
hiyo ambayo waliifananisha na send off.
Imeelezwa kuwa, baada ya
kumalizika kwa sherehe hiyo Diamond alimtumia Penny salamu za pongezi
akiwa Uingereza na kumuahidi kumletea bonge la zawadi pindi atakaporejea
Bongo.
Mbali na ndugu, jamaa na marafiki wa mastaa hao kuhudhuria, mastaa mbalimbali wa filamu na muziki walitokea kumuunga mkono akiwemo Mtangazaji wa Televisheni ya Star TV, Sauda Mwilima na Rommy Jonson ambaye ni kaka’ke na Diamond.

No comments:
Post a Comment