STAA wa filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amelipuka na kudai kuwa
wasanii wa filamu wa Tanzania wanakandamizwa sana na wasambazaji.
Akizungumza hivi karibuni katika mahojiano maalum, Ray alisema: “Kama
nitakuwa sijajifunza kitu kutokana na msiba wa Kanumba (Steven) nitakuwa
mjinga. Kama utakumbuka, kwenye mazishi yake serikali nzima ilikuwa
pale, umati mkubwa wa watu ulifurika, kwa nini? Kwa sababu ya thamani
yake.
“Msambazaji aliye ‘serious’ ni mmoja kwa sasa na yeye ndiye
anayeamua cha kufanya na kwa sababu wasanii tupo wengi, hatuna jinsi.
Ukiingia naye mkataba unakuwa umeuza haki ya maisha yako yote. Anakuwa
na uhuru wa kupeleka DSTV, Zuku na Channel nyingine zozote bila kukulipa
chochote.
“Lakini mimi siwezi kutupa lawama kwa serikali maana
tumeshaongea sana. Nawaomba wadau wajitokeze wawekeze kwenye tasnia yetu
maana inapanuka na ina soko kubwa ila msambazaji yupo mmoja tu ndiyo
maana tunanyonywa.”
No comments:
Post a Comment