Dodoma.
Serikali imeita mifuko ya hifadhi ya jamii kutogombea wanachama, badala yake watafute wapya.
Akizungumza katika semina kuhusu mifuko ya Hifadhi
ya Jamii jana, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Milton Makongoro
alisema mifuko hiyo haina haja ya kugombania wanachama kwani hata
waliopo hawatoshelezi.
Dk Makongoro alisema hivi sasa wanachama ni
milioni 1.2 sawa na asilimia tatu kati ya sita ya nguvu kazi, ambao ni
watu milioni 23.
“Kuna kila sababu ya viongozi wa Mifuko ya Hifadhi
ya Jamii kuhakikisha wanatafuta wanachama wapya, badala ya
kunyang’anyana wanachama kuna watu wengi ambao hawajajiunga,” alisema Dk
Makongoro.
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irine Isaka alisema
mamlaka hiyo imeweka utaratibu wa kuhakikisha hakuna urasimu wa huduma
za mifuko hiyo.
“Zamani mifuko mingi ilikuwa na urasimu wa
kuhudumia wanachama kwa kuweka matabaka, lakini sasa hali hiyo imeisha,”
alisema Isaka.
Wakati huohuo, Rais Jakaya Kikwete antafungua maonyesho mifuko hiyo.
No comments:
Post a Comment