Kwa mujibu wa msemaji wa Kampuni ya Kowack Brothers inayoratibu
shindano hilo, Aneth Makagua, kila mrembo ana shauku kubwa ya kuibuka
mshindi na kubeba zawadi.
Aneth alisema zawadi kwa mshindi ni sh 400,000 na sofa yenye thamani
zaidi ya kiasi hicho huku wengine wakiondoka na zawadi kemkemu.
“Warembo siku hiyo watapita jukwaani kuonesha urembo na umahiri wao wa
mambo mbalimbali kama mitindo na shoo ili kutoa nafasi kwa majaji
kuchagua mshindi,” alisema Aneth.
Kuhusu kiingilio, alisema kitakuwa sh 10,000 kwa viti vya kawaida na
sh 20,000 kwa viti maalumu na kuongeza kuwa, bendi ya Twanga Pepeta
ndiyo itaporomosha burudani.
Naye Mkurugenzi wa Kowack Brothers, Osango Appollo, amewasihi wadau
kujitokeza kushuhudia fainali hiyo akisema itakuwa ya kiwango bora.
“Tumepania kufanya makubwa katika kuhakikisha tunatoa warembo bomba
ambao watakuwa tishio katika ngazi za juu kuanzia ambazo ni mkoa, kanda
hadi taifa,” alisema.
Shindano hilo linafanyika chini ya wadhamini Club Bilicanas, Tesco
Funiture, kinywaji cha Chill Will, Tanzania Daima, CXC Africa, Gogo
shop, Lakairo Investment, Lamada Hotel, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
kupitia kinywaji cha Redd’s na wengineo.
No comments:
Post a Comment