Manchester, England.
Alex Ferguson ataendelea kuwa taswira ya uendeshaji wa timu ya Manchester United hata baada ya kutangaza kujiuzulu mwishoni mwa msimu, baada ya uongozi wa klabu hiyo kukubali pendekezo lake la kutaka Kocha David Moyes kurithi mikoba yake.
Alex Ferguson ataendelea kuwa taswira ya uendeshaji wa timu ya Manchester United hata baada ya kutangaza kujiuzulu mwishoni mwa msimu, baada ya uongozi wa klabu hiyo kukubali pendekezo lake la kutaka Kocha David Moyes kurithi mikoba yake.
Moyes, bosi wa Everton alitangaza juzi kuwa
ataondoka kwenye klabu hiyo baada ya miaka 11 na anatarajia kujiunga
rasmi na United Julai Mosi mwaka huu.
“Tulipojadili kuhusu kocha mwenye uwezo kufundisha United, mara moja tulikubaliana awe David Moyes,” alisema Ferguson, ambaye baada ya kujiuzulu atabaki kama balozi na mkurugenzi wa klabu.
“David ni mtu mwelevu, mwenye msimamo na maadili. Siku zote nimekuwa nikifurahishwa na kazi yake tangu mwaka 1998 tulipozungumza juu ya kuwa kocha msaidizi United.
“Wakati huo alikuwa kijana mdogo na tangu wakati huo amefanya kazi nzuri Everton. Hakuna maswali, ana sifa zote za kuitwa kocha kwenye klabu hii.”
“Siku zote nimekuwa nikieleza kwamba nahitaji kuona kocha ajaye kweli mtu wa Manchester United,” alisema Ferguson.
Moyes anachukua nafasi ya Ferguson, kocha mwenye mafanikio katika historia soka la England, akitwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mataji 13 Ligi Kuu England, mataji matano FA katika miaka 26.
“Moyes atabaki kuifundisha Everton michezo miwili
iliyobaki kabla ya kumalizika msimu dhidi ya West Ham na Chelsea kisha
ndipo atakapojiunga na United.
No comments:
Post a Comment