Dar es Salaam.
Wakati Uongozi wa Yanga ukitenga sh150 milioni kwa wachezaji iwapo watawafunga wapinzani wao Simba, kikosi cha timu hiyo kimeondoka jana kwa mafungu kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kambi.
Wakati Uongozi wa Yanga ukitenga sh150 milioni kwa wachezaji iwapo watawafunga wapinzani wao Simba, kikosi cha timu hiyo kimeondoka jana kwa mafungu kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kambi.
Habari za uhakika ambazo Mwananchi ilizipata na kushuhudia wachezaji wa Yanga wakiingia kwenye Coasta la klabu hiyo waliyopewa na wadhamini wao Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ilisema kuwa wachezaji hao walikuwa wanaelekea Pemba ambapo watakuwa wakifanya mazoezi kwenye uwanja wa Gombani.
“Fungu la kwanza limeondoka asubuhi majira ya saa tano, lilikuwa na wachezaji kama Simon Msuva, Shedrack
Nsajigwa na wengine, fungu la pili ni hili la kina Chuji na wenzake wakina Nurdin ambalo litaondoka saa tisa na fungu la tatu litaondoka kesho asubuhi.”alisema mmoja wa viongozi ndani ya klabu hiyo.
Yanga ilikuwa ikidai itaweka kambi Makao Makuu ya
Klabu hiyo iliyopo mtaa wa Twiga na Jangwani na kile walichokuwa
wakikieleza kuwa mechi hiyo haina umuhimu kwao kwani ni ya kukamilisha
ratiba.
“Awali uongozi uliaidi kama watafanikiwa kushinda mechi zote za lala salama basi watapewa milioni100 na wiki iliyopita wamewaongezea milioni50 iwapo watafanikiwa kumfunga Simba.
Iwapo uongozi huo wa Yanga itatoa kiasi hicho cha fedha basi kila mchezaji atakuwa amevuna shilingi5 milioni.
No comments:
Post a Comment