KLABU ya Tout Puissant
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambayo inajivunia
washambuliaji wawili wa Kitanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu
itamenyana na Liga Maculmana ya Msumbiji kuwania tiketi ya kucheza hatua ya
makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Hiyo inafuatia upangwaji wa droo ya hatua
ya 16 Bora ya michuano hiyo, inayodhaminiwa na Orange mjini Cairo, Misri leo.
Katika droo hiyo, AS FAR Rabat ya Morocco iliyoitoa Azam FC katika Kombe la
Shirikisho imepangwa kukutana na wapinzani wao, FUS Rabat. Katibu Mkuu wa CAF,
Hicham El Amrani aliongoza droo hiyo kwa pamoja na wawakilishi wa baadhi ya
klabu zinazoshiriki michuano hiyo.
Klabu nane zilizotolewa katika Ligi ya
Mabingwa, St George, CA Bizerte, TP Mazembe, Enugu Rangers, JSM Bejaia, FUS
Rabat, Stade Malien na Entente Setif zimeingia kwenye mbio za kuwania kurithi
taji la AC Leopards ya Kongo, mabingwa wa Kombe la Shirikisho na mechi za kwanza
zitachezwa kati ya Mei 17, 18 na 19 mwaka huu wakati marudiano yatakuwa kati ya
Mei 31 , Juni 1 na 2. Mazembe ambao ni mabingwa mara nne Afrika, walitolewa na
Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika Raundi ya Tatu ya Ligi ya Mabingwa kwa
jumla ya mabao 3-2, wakifungwa 3-1 Afrika Kusini na kushinda 1-0
nyumbani.
DROO KAMILI YA 16 BORA KOMBE LA SHIRIKISHO:
Stade Malien (Mali) vs Lydia (Burundi)
Enugu Rangers ( Nigeria) vs C.S.S (Tunisia)
FUS Rabat ( Morocco) vs ASFAR (Morocco)
CAB (Tunisia) vs Ismailia (Misri)
E.S Setif ( Algeria) vs US Bitam (Gabon)
JSM Bejaia ( Algeria) vs E.S.S (Tunisia)
TP Mazembe (DRC) vs Liga Maculmana (Msumbiji)
St George (Ethiopia) vs ENPPI (Misri)
DROO KAMILI YA 16 BORA KOMBE LA SHIRIKISHO:
Stade Malien (Mali) vs Lydia (Burundi)
Enugu Rangers ( Nigeria) vs C.S.S (Tunisia)
FUS Rabat ( Morocco) vs ASFAR (Morocco)
CAB (Tunisia) vs Ismailia (Misri)
E.S Setif ( Algeria) vs US Bitam (Gabon)
JSM Bejaia ( Algeria) vs E.S.S (Tunisia)
TP Mazembe (DRC) vs Liga Maculmana (Msumbiji)
St George (Ethiopia) vs ENPPI (Misri)
No comments:
Post a Comment