Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi juzi aliwaondolea
uvivu wapinzani na kuwaeleza kuwa hawezi kujiuzulu wala kufanya kazi kwa
shinikizo la wanasiasa.
Mbali na hilo, aliwataka wapinzani kugombea
na kupata nafasi za urais ili waweze kuweka utaratibu wa kuwafukuza
mawaziri wao watakaoona hawafanyi kazi ipasavyo.
Nchimbi alitoa kauli hiyo wakati akijibu hoja kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mwaka 2013/14.
Nchimbi alitoa kauli hiyo wakati akijibu hoja kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mwaka 2013/14.
“Nataka kumwambia ndugu
yangu Lissu kuwa, kazi ya wagombea wote ni kuomba ridhaa ya kuchaguliwa
ili waweze kuweka taratibu za kuajiri na kufukuza,hivyo ili kumwondoa
waziri, nawashauri nanyi mgombee urais na mpate ili mjiweke katika
nafasi ya kufukuzana,” alisema Nchimbi.
Alimsifia Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda kuwa anafanya kazi nzuri licha ya
malalamiko yanayotolea na wanasiasa na baadhi ya wanaharakati na kusema
hatakiwa kuacha kazi hiyo kwa shinikizo hizo.
Hata hivyo alikubaliana
na hoja iliyotolewa na msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Vicent
Nyerere kuwa kuna silaha nyingi ambazo zimezagaa nchini.
“Hilo nakubaliana nalo, kuna ongezeko la silaha nyingi nchini jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa raia wetu,mbali na hilo pia nachukizwa na vitendo vya rushwa ndani ya jeshi la polisi”.
Alisema Serikali imejipanga vizuri kwa ajili ya kukabiliana na vitendo hivyo na kuwawajibisha askari wake ambao si waaminifu ndani ya jeshi

No comments:
Post a Comment