
KOCHA wa Taifa Stars, Kim Poulsen, amesema watahakikisha wanashambulia
mwanzo mwisho kwenye mechi ya kuwania kufunzu Kombe la Dunia 2014 dhidi
ya Morocco, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Marrakesh, Morocco.
Boniface
Wambura ambaye ni Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
ameliambia gazeti hili kuwa, Kim amepanga kutumia mfumo wa kushambulia
mwanzo mwisho ili ahakikishe wanafunga mabao ya mapema zaidi.
“Kocha
anasema kuwa atatumia mfumo wa kushambulia mwanzo mwisho lengo ni kupata
mabao ya mapema zaidi na kisha kuyalinda katika kipindi cha pili.
“Wachezaji
wote wapo fiti, (Erasto) Nyoni amerejea na alifanya mazoezi kama
kawaida lakini mwalimu anatarajia kumuanzisha (Thomas) Ulimwengu ambaye
atacheza pacha na (Mbwana) Samatta, tutarejea nyumbani Jumapili,”
alisema Wambura.
No comments:
Post a Comment