Deni
la Taifa limekua hadi kufikia Sh. bilioni 21,028.61 hadi kufikia
Desemba mwaka jana ikilinganishwa na Sh. bilioni 18,258.62 Desemba mwaka
2011.
Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Rais, (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira, aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi kwa mwaka 2012 na Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2013/2014.
Wassira alisema kati ya kiasi hicho cha fedha Sh. bilioni 19,692.5 ni deni la serikali wakati Sh.bilioni 3,019.4 ni deni la sekta binafsi.
“Ongezeko hilo linatokana na mikopo mipya yenye masharti nafuu na kibiashara na malimbikizo ya riba ya deni la nje hasa kwenye nchi zisizo wanachama wa kundi la Paris ambazo hazijajitoa katika msamaha,” alisema.
MATUMIZI YA SERIKALI
Wassira alisema katika kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka jana, matumizi ya serikali yalikuwa ni Sh. bilioni 7,252.3 sawa na asilimia 95 ya makadirio ya shilingi bilioni 7,634.00.
Alisema kati ya fedha hizo Sh. bilioni 5,247.5 na matumizi ya maendeleo yalikuwa ni shilingi bilioni 2,004.9.
MIKOPO
Wassira alisema katika kipindi cha kati ya Julai hadi Desemba mwaka jana, Serikali ilipokea msaada na mikopo ya kibajeti ya jumla ya Sh. bilioni 564.2 sawa na asilimia 67 ya makadirio ya sh. bilioni 842.5 katika kipindi hicho.
Pia katika kipindi hicho Sh. bilioni 438.1 zilipokelewa kupitia mifuko ya kisekta ikiwa ni sawa na asilimia 106 ya makadirio ya Sh. bilioni 415.1 katika kipindi hicho.
Wassira alisema katika kipindi hicho misaada na mikopo nafuu
iliyopokelewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa kipindi cha Julai
hadi Desemba mwaka jana ilifikia Sh. bilioni 617.5 ambayo sawa na
asilimia 33 ya ahadi ya Sh.bilioni 1,899.1 katika kipindi hicho katika
kipindi hicho kwa mwaka 2012/13.Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Rais, (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira, aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi kwa mwaka 2012 na Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2013/2014.
Wassira alisema kati ya kiasi hicho cha fedha Sh. bilioni 19,692.5 ni deni la serikali wakati Sh.bilioni 3,019.4 ni deni la sekta binafsi.
“Ongezeko hilo linatokana na mikopo mipya yenye masharti nafuu na kibiashara na malimbikizo ya riba ya deni la nje hasa kwenye nchi zisizo wanachama wa kundi la Paris ambazo hazijajitoa katika msamaha,” alisema.
MATUMIZI YA SERIKALI
Wassira alisema katika kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka jana, matumizi ya serikali yalikuwa ni Sh. bilioni 7,252.3 sawa na asilimia 95 ya makadirio ya shilingi bilioni 7,634.00.
Alisema kati ya fedha hizo Sh. bilioni 5,247.5 na matumizi ya maendeleo yalikuwa ni shilingi bilioni 2,004.9.
MIKOPO
Wassira alisema katika kipindi cha kati ya Julai hadi Desemba mwaka jana, Serikali ilipokea msaada na mikopo ya kibajeti ya jumla ya Sh. bilioni 564.2 sawa na asilimia 67 ya makadirio ya sh. bilioni 842.5 katika kipindi hicho.
Pia katika kipindi hicho Sh. bilioni 438.1 zilipokelewa kupitia mifuko ya kisekta ikiwa ni sawa na asilimia 106 ya makadirio ya Sh. bilioni 415.1 katika kipindi hicho.
AKIBA YA FEDHA ZA NJE
Wassira alisema katika kipindi kilichoishia Desemba mwaka ja, akiba ya fedha za kigeni ilikuwa ni dola za kimarekani milioni 4,069.1 ikilinganishwa na Dola za Kimarekani 3,761.2 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2011.
“Kiasi hiki ni cha akiba ya fedha za kigeni kwa mwaka 2012 kinatosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa miezi 3.9 ikilinganishwa na miezi 3.8 iliyofikiwa mwaka 2011,”alisema.
UKUAJI WA PATO
Waziri huyo alisema mwaka 2012 pato la Taifa lilikuwa Sh.milioni 44,717,663 ikilinganishwa na Sh. milioni 37,532,962 mwaka 2011.
Pia alisema wastani wa pato la kila mtu liliongezeka kwa asilimia 17.9 na kuwa Sh. 1,025,038 mwaka jana ikinganishwa na Sh.869,436.3 mwaka 2011.
Kwa mujibu wa Wassira nchi za Tanzania na Kenya zimeonyesha ukuaji mzuri wa uchumi ikilinganishwa na Rwanda, Burundi na Uganda kwa mwaka 2012.
AJIRA
Alisema kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana nchini ni asilimia 8.8 ambayo ni karibu mara mbili ya kiwango cha jumla cha ukosefu wa ajira kwa Taifa asilimia 4.7.
Hata hivyo, Wassira alisema jumla ya nafasi ya ajira 250,678 zilipatikana katika maeneo ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), ujenzi wa barabara, ujenzi wa majengo ya serikali na uwekezaji kupitia Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC).
Nyingine ni EPZA, serikali, miradi ya kilimo, Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Vidogo (Sido), miradi ya maji, kampuni nyingine toka ofisi za ajira za mikoa.
MPANGO WA MAENDELEO
Wassira alisema katika kugharamia mipango ya maendeleo wa miaka mitano ilikadiriwa kuwa shilingi trilioni 8.9 zitahitajika kila mwaka, kati ya hizo Sh. trilioni 2.9 zitatokana na fedha za ndani katika bajeti ya serikali.
Alisema pia Sh. trilioni 2.9 zilitokana na fedha za ndani katika bajeti ya serikali na shilingi trilioni 6.0 zilizotokana na uwekezaji wa sekta binafsi na washirika wa maendeleo.
Alisema katika mwaka 2013/2014 serikali imekadiria kutumia Sh. trilioni 5.67 sawa na asilimia 31.09 ya bajeti yote kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kati ya fedha hizo Sh. trilioni 2.69 ni fedha za nje na Sh.trilioni 2.98 ni fedha za ndani Wassira alisema mwendelezo wa utekelezaji wa miradi na program mbalimbali zilizoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano (2011/12-2015/16).
Alisema vipaumbele vitaendelea kuwa ni vile vile vya mpango wa miaka mitano ambavyo ni miundombinu, kilimo, viwanda, maendeleo ya raslimali watu na uendelezaji wa huduma za utalii, biashara na fedha.
Alisema shabaha na malengo ya kiuchumi katika mwaka wa fedha 2013/2014 ni kuongeza kasi ya ukuaji wa pato halisi la Taifa kutoka asilimia 6.9 mwaka 2012, asilimia 7.0 mwaka 2013 , asilimia 7.5 mwaka 2014, asilimia 8 mwaka 2015.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment