Mgombea udiwani Kata ya Elerai Manispaa ya Arusha
kwa tiketi ya Chama cha Tanzania Labour(TLP), Boysafi Peter Shirima
jana alitangaza kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho na kujiunga na
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa
Akitangaza uamuzi huo mbele ya umati wa watu, waliohudhuria mkutano wa
hadhara wa kampeni zinazoendelea katika kata hiyo, alidai kuwa amejitoa
katika chama hicho kutokana na chama kushindwa kuzindua kampeni za
kumnadi licha ya kuwa mgombea kwa mkoa mzima wa Arusha.
“Mimi ni mgombea pekee kwa chama hiki kwa sababu ni peke yangu niliyesimama kwa nia dhabiti na kupeperusha bendera ya TLP lakini viongozi wa chama hiki wameshindwa kabisa kunipa ushirikiano... sasa naondoka na naomba wapiga kura wangu wote pigieni Chadema (Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),”alisema.
Alisema sababu nyingine iliyomwondoa katika chama hicho ni kukosa ushirikiano kwa viongozi na kumwacha peke yake kunadi sera za TLP.
Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, alisema chama icho kimefurahishwa kuona mgombea huyo ameamua mapema
kujisalimisha mahali salama na kuondokana na propaganda na kwamba wanamkaribisha kwa mikoni miwili wawatumikie wananchi.
“Huyu mgombea amesikiliza Chadema ameona sera na maneno yetu yanaendana na ukweli na siyo kama vyama vingine wanaongea mengine
lakini matendo tofauti... tunamkaribisha kupigania haki za wananchi,”alisema.
Baada ya Shirima kujiengua katika kinyanyang'anyito hicho, Mhandisi Jeremiah Mpinga wa Chadema sasa atachukuana wagombea vyama vya CUF na CCM.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment