MTANGAZAJI wa Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amefungua kinywa
chake na kusema ugonjwa wa malaria uliompata hivi karibuni ulimfanya
alichungulie kaburi kwani alihisi mauti yanamkuta.
Akizungumza na paparazi wetu mapema wiki hii katika Hospitali ya
Muhimbili, jijini Dar, Dida alisema kitendo cha kukutwa na malaria 250
katika mwili wake kilikuwa hatari sana kwani ingeweza kumuondoa uhai
kabisa.
“Nilichungulia kaburi mwenzenu maana hali niliyokuwa naisikia
siku ile ya kwanza ilikuwa ni nusu duniani, nusu akhera. Nilikuwa wa
leo au wa kesho ila namshukuru Mungu kwa sasa naendelea vizuri,” alisema
Dida.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Dida alipandwa na malaria kali,
akakimbizwa katika Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar kisha
kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment