Ethiopia na Misri wamekubaliana kufanya mazungumzo ya ziada juu ya
athari za bwawa kubwa ambalo Ethiopia inalijenga kwenye mto Nile.
Wiki iliyopita Rais wa Misri, Mohammed Morsi alisema hataki vita lakini ataweka mapendekezo yote wazi yanayohusu majibu ya nchi yake kwa mradi wa bwawa hilo ambalo Misri inawasi wasi utapunguza sana kiwango cha usambasaji wake wa maji.
Maafisa wa Ethiopia walijibu wakisema hawatasitisha ujenzi wa bwawa la Grand Ethiopian Renaissance Dam wenye gharama ya takribani dola bilioni 5.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Mohamed Kamel Amr alisema Jumanne kwamba taarifa zilizotolewa awali zilitokana na “jazba za wakati huo”.
Amr alikutana na kiongozi mwenzake wa Ethiopia, Tedros Adhanom, siku ya
Jumatatu na Jumanne katika mji mkuu wa Ethiopia. Wote walisema
wataendelea na mazungumzo kuhusu bwawa la usambazaji umeme ikiwemo
mazungumzo zaidi ya kiufundi.Wiki iliyopita Rais wa Misri, Mohammed Morsi alisema hataki vita lakini ataweka mapendekezo yote wazi yanayohusu majibu ya nchi yake kwa mradi wa bwawa hilo ambalo Misri inawasi wasi utapunguza sana kiwango cha usambasaji wake wa maji.
Maafisa wa Ethiopia walijibu wakisema hawatasitisha ujenzi wa bwawa la Grand Ethiopian Renaissance Dam wenye gharama ya takribani dola bilioni 5.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Mohamed Kamel Amr alisema Jumanne kwamba taarifa zilizotolewa awali zilitokana na “jazba za wakati huo”.
Sehemu kubwa ya maji ya mkondo wa mto Blue Nile yanaanzia nchini Ethiopia. Hata hivyo mikataba ya enzi za ukoloni iliyoandikwa na Uingereza inaipa Misri asilimia 87 ya mtiririko wa maji ya mto Nile.
No comments:
Post a Comment