Mkuu
wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye akiongea machache
wakati kamati hiyo ilipotembelea Kambi ya Mazoezi ya Redds Miss
Kinondoni 2013 iliyopo katika hoteli ya JB Belmont hoteli jijini Dar es
Salaam. Kutoka upande wa mkuu wa Itifaki ni katibu Bosco Majaliwa,
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega, mjumbe wa kamati
hiyo, Lucas Rutta wakiwa pamoja muandaaji wa mashindano hayo Dennis
Ssebo.
Mkurugenzi
wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega, akiongea na warembo
wanaowania taji la Redds Miss Kinondoni 2013 mara baada ya kuwatembelea
kambini kwao na kujua wanaendeleaje. Lundenga aliwaasa washiriki hao
kuongeza bidii katika mazoezi yao ili waweze kufanya vyema katika
fainali yao.
Na Cathbert Angelo, Kajunason Blog
Kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi Hashimu Lundenga imetembelea kambi ya Redds Miss Kinondoni 2013 wanaotarajiwa kumenyana leo alhamisi (leo) ya Juni 20 katika shindano Redd’s Miss Kinondoni Talent 2013 katika ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mratibu wa shindano hilo mara baada ya kuwakaribisha
wageni, Dennis Ssebo alisema maandalizi ya kuelekea shindano hilo
yanaendelea vizuri na kueleza mshindi atakabidhiwa zawadi zake kwenye
fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika Juni 21 mwaka huu katika
uwanja wa hoteli ya Golden Tulip.
Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya
urembo kwa wilaya ya Kinondoni maana wamejipanga na kupata sapoti ya
kutosha, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata
raha.
Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Kiota cha Maraha WANTASH, Virago, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, TheHabari.com, JestinaGeorge Blog, Sufian Mafoto Blog, Global Publishers, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.

No comments:
Post a Comment