Sauti yake ipo hapa soundcloud.com
Anakwambia ‘Twende Kigoma, Mwanza, Tabora, Mpanda, Shinyanga
tuwaulize watu mnataka reli au viwanja vya ndege… mtashangaa wenyewe,
vipaumbele gani mnapeleka viwanja vya ndege? mtu gani wa Tabora anapanda
ndege kama sio Mbunge, DC na Mkuu wa mkoa… ? ni Treni…… hawataki
viwanja vya ndege, viwanja vya ndege baadae…. kwanza ndege zenyewe
zikwapi? mna ndege nyie???? mabilioni ya hela mnajenga viwanja vya
ndege… ndege hatuna, wapanda ndege ni nyie wenyewe Wabunge na Mawaziri…
jamani tutulie tuweke vipaumbele ambavyo vinaweza kusaidia Wananchi na
uchumi wa nchi, mtapakia mizigo, madebe mawese kwenye ndege? migebuka
kwenye ndege? acheni mambo ya kurukiakurukia ndege zenyewe hamna”
“Mmefilisi shirika la ndege tunawaambia tuwakamate wale
waliofilisi tuwafunge pingu zao, sasa sheria mpya kama wamekufa
tuwafufue tuwasage mifupa yao… mi nashangaa baadhi ya Wabunge hapa
wanakuja tuondoe hela hii tuondoe hela hii… utapata wapi hela ya
kuiendeleza nchi yako? leo Uingereza kodi ya TV unalipia, ukiwa nazo
tatu utalipia kila moja… wewe una TV mpaka 10 mpaka chooni, umekaa
hulipii chochote… nani akudai? ” – Keissy
“Mafisadi wanajulikana, hata mzee Sitta nimemsikia siku moja
akisema hawa dawa yao kuwanyonga….. mimi Mbunge hapa, baada ya mwaka
nina gorofa 10 nimepata wapi hela? sijakwenda benki sijakwenda popote,
hapohapo ndio pa kunibana… na hizi pesa zinazochangiwa kwenye maharusi
mabilioni ya hela, michango ya kanisa na Misikiti zikatwe kodi 30%
palepale… wauza dawa za kulevya kama hawajakamatwa lakini wana majumba,
wakatwe kodi.. shida yetu kodi sisi hatujui dawa zako umepeleka wapi
huko tumeshindwa kukukamata lakini tulipe kodi” – Mbunge Keissy
“Tukipata maafa kidogo… kelele misaada, tukisema kodi mnapiga
kelele nyie Wabunge… Ebooooo? itakuaje? nani ameoa Mwanamke nyumbani
kwake anakwenda kuomba msaada kwa jirani? watakuchukulia mke wako…
JITEGEMEE!!!!!”
Watu mbavu hawana…… unaweza kumsikiliza mwenyewe hapa chini upate uhondo wote
No comments:
Post a Comment