SHIRIKISHO la Muziki Tanzania, limesema kuwa mwili wa aliyekuwa
mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Albert Mangwea ‘Ngwair’, sasa
unatarajiwa kuwasili leo mchana.
Mwili wa msanii huyo aliyefariki Mei 28 nchini Afrika Kusini, umekuwa ukipigwa danadana ujio wake, kila ulipotangazwa.
Rais wa Shirikisho hilo, Ado Novemba, alisema kwamba mwili huo unatarajiwa kuwasili leo majira ya saa nane mchana.
Alisema kwa sasa kila kitu kiko tayari, hivyo mwili ukifika utaagwa
siku utakayofika na baadaye atakwenda kuzikwa nyumbani kwao Kihonda
mkoani Morogoro.
Ngwair, alizaliwa 1982 na nyota yake ilianza kuchomoza katika kundi la East Zoo mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment