KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts ameanza kazi ya kukinoa kikosi chake,
lakini katika siku ya kwanza akawapokea nyota wawili muhimu ambao wote
wanatoka katika Klabu ya Simba.
Brandts alitua nchini juzi akitokea
Uholanzi alikokwenda kwa ajili ya mapumziko mafupi, mara baada tu ya
kikosi chake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita.
Kwa sasa anaiandaa Yanga kwa ajili ya michuano ya Kombe la Kagame itakayochezwa kuanzia Juni 18, mwaka huu nchini Sudan.
Kwa sasa anaiandaa Yanga kwa ajili ya michuano ya Kombe la Kagame itakayochezwa kuanzia Juni 18, mwaka huu nchini Sudan.
Katika
mazoezi hayo yaliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari
Loyola iliyopo Mabibo jijini Dar, Brandts alikabidhiwa straika Shaban
Kondo na beki Rajab Isihaka.
Kondo alisajiliwa na Yanga wiki hii akitokea Simba ambako aliishia kufanya mazoezi ya kujaribiwa kabla Yanga hawajamuona na kumsainisha mkataba wa miaka mitatu ‘fasta’ huku Simba wakiachwa
Kondo alisajiliwa na Yanga wiki hii akitokea Simba ambako aliishia kufanya mazoezi ya kujaribiwa kabla Yanga hawajamuona na kumsainisha mkataba wa miaka mitatu ‘fasta’ huku Simba wakiachwa
wameshika vichwa wasijue la kufanya.
Kufuatia hatua hiyo,
Championi Ijumaa lilimtafuta Brandts mara baada ya mazoezi hayo, ambapo
licha ya kufurahishwa na uwezo wa nyota hao, aliomba apewe muda zaidi
kabla ya kuwatolea tathmini sahihi.
“Nimewaona, ni wachezaji wazuri,
leo (jana) ni siku moja tu tangu nimewaona, nafikiri nipewe muda nikae
nao hata kwa wiki moja ili niweze kutoa majibu mazuri zaidi lakini kwa
haraka naweza kusema ni wachezaji wazuri,” alisema Brand
No comments:
Post a Comment