Charles ambaye pia alikuwa bingwa wa
mashindano ya mbio za baiskeli yaliyofanyika Arusha mwaka jana,
anatuhumiwa kufanya mauaji ya ukatili wilayani Mpanda. Inaelezwa kuwa
kwa zaidi ya miaka 15, Charles amekuwa akishiriki katika mashindano ya
mbio za baiskeli katika mikoa ya Tabora, Shinyanga, Mwanza na Arusha
Oktoba mwaka jana ambako aliibuka mshindi na kujinyakulia Sh 800,000.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari, mtuhumiwa huyo ni mkazi wa Kijiji cha Chilalo Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Charles anatuhumiwa kumuua Moshi Bella (44) wa Kijiji cha Karema kwa kumkatakata na panga kichwani na shingoni baada ya kuahidiwa kulipwa Sh milioni tano.
Kamanda Kidavashari alisema tukio hilo la mauaji ya kinyama lilitokea Julai 21 mwaka huu katika Kijiji cha Kabange Kata ya Simbwesa Tarafa ya Kabungu mkoani Katavi.
Alisema mtuhumiwa kabla ya kufanya mauaji hayo alionana na Bella akijifanya alikuwa anataka auziwe shamba.
Mazungumzo
hayo yalifanyika Julai 20 mwaka huu nyumbani kwa Salumu Kajimba ambaye
ni ndugu wa marehemu Bella, alisema Kamanda Kidavashari.Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari, mtuhumiwa huyo ni mkazi wa Kijiji cha Chilalo Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Charles anatuhumiwa kumuua Moshi Bella (44) wa Kijiji cha Karema kwa kumkatakata na panga kichwani na shingoni baada ya kuahidiwa kulipwa Sh milioni tano.
Kamanda Kidavashari alisema tukio hilo la mauaji ya kinyama lilitokea Julai 21 mwaka huu katika Kijiji cha Kabange Kata ya Simbwesa Tarafa ya Kabungu mkoani Katavi.
Alisema mtuhumiwa kabla ya kufanya mauaji hayo alionana na Bella akijifanya alikuwa anataka auziwe shamba.
Kamanda alisema mtuhumiwa na Bella walikubaliana kuuziana ekari mbili za shamba ambalo ni mbuga ya mpunga.
“Walikubaliana kuuziana Sh 300,000 kwa kila ekari na baada ya makubaliano hayo mtuhumiwa alimuahidi Bella kwamba angerejea siku ya pili kwa ajili ya kutoa malipo hayo,” alisema Kamanda.
Alisema siku iliyofuata mtuhumiwa Charles alifika nyumbani kwa Salumu Kajimba ambaye ni ndugu wa Bella ya saa 9.00 alasiri lakini bahati mbaya Bella alikuwa amekwenda kisimani kuoga.
Mtuhumiwa baada ya kuambiwa Bella alikuwa amekwenda kisimani alimuaga Kajimba na mkewe akisema alikuwa anamfuata Bella.
Kamanda Kidavashari alisema Bella hakuonekana nyumbani tangu alivyowaaga kuwa anakwenda kuoga kisimani wala Bella aliyemfuata naye hakurejea hadi hapo mwili wa Bella ulipookotwa mbugani.
Mwili wa Bella ulikutwa umekatwakatwa na panga shingoni kwa nyuma na kichwani.
Kamanda alisema baada ya polisi kuarifiwa na raia wema kuhusu mauaji hayo waliweza kumkamata mtuhumiwa Masaga Charles katika mtaa wa Makanyagio mjini Mpanda.
Baada ya kukamatwa mtuhumiwa alikiri kuhusika na mauaji hayo akidai alitumwa na mkazi mmoja wa Kijiji cha Iroba Tarafa ya Kabungu wilayani Mpanda aliyemuahidi kumlipa Sh milioni tano.
Kamanda alisema mtuhumiwa alidai kuwa mtu aliyemtuma amekwisha kukimbilia mkoani Shinyanga ili asijulikane kuwa ndiye aliyehusika na mpango wa mauaji hayo.
Mtuhumiwa alidai kuwa kwa mara ya kwanza aliambiwa kufanya mauaji hayo Oktoba mwaka jana kwa malipo ya Sh milioni mbili lakini alikataa, alisema. Kamanda alisema mtuhimiwa alidai kuwa Aprili mwaka huu aliambiwa tena afanye mauaji kwa malipo hayo lakini akaendelea kukataa hadi alipoongezewa dau na kufika Sh milioni tano na kupewa shamba la ekari mbili.
Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma za mauaji zinazomkabili, alisema kamanda.
CHANZO CHA HABARI NI MTANZANIA
No comments:
Post a Comment