MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imesema taarifa
zaidi kuhusu kesi ya kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka, itatolewa Agosti 6 mwaka huu.
Hayo yalisemwa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Waliarwande Lema,
wakati kesi hiyo ilipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.
“Taarifa zaidi za shauri lako zitatolewa Agosti 6 mwaka huu na mshitakiwa utaendelea kubaki rumande,”alisema Hakimu Lema.
Mara ya mwisho, kesi hiyo ilipotajwa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu iliiahirisha kwa mara ya mwisho kutokana na upande wa mashtaka kueleza kwamba bado unaendelea na upelelezi wa shauri hilo.
Hakimu Lema aliutaka upande huo kukamilisha upelelezi wake ifikapo jana kesi hiyo ilipotajwa tena mahakamani hapo.
Katika kesi hiyo, mtuhumiwa Joshua Mulundi, ambaye ni raia wa Kenya, anatuhumiwa kuhusika na tukio la kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka.
Wakati huo huo, leo mahakama hiyo inatarajia kutoa hukumu dhidi ya Wachungaji waliokuwa wakiendesha biashara ya Upatu bila kibali.

VIA MTANZANIA
No comments:
Post a Comment