*Atangaza wiki mbili msako wa silaha mikoa mitatu
*Asema wakishindwa JWTZ, Polisi wataingia kazini
RAIS Jakaya Kikwete, ametangaza msimamo mkali baada ya kutoa wiki mbili kwa watu wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria katika mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma kuzisalimisha kwa hiari yao kabla ya kutiwa mbaroni.
Rais Kikwete, ametoa kauli hiyo wilayani Biharamulo mkoani Kagera jana, wakati akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 154, kutoka Kagoma hadi Rusaunga. Alisema baada ya wiki mbili kupita, Serikali itaanzisha operesheni maalumu kusaka silaha hizo kwa kupita nyumba hadi nyumba.
Alisema operesheni hiyo maalumu, itaendeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa.
"Sitakubali kuona Watanzania waishi kama wakimbizi katika nchi yao… nitahakikisha silaha zote zinazomilikiwa kinyume na sheria zinasakwa zote na wamiliki wa silaha hizo wanakamatwa," alisema Rais Kikwete.
Alisema operesheni hiyo, haitaangalia mtu usoni awe Mtanzania au raia wa nje ya nchi.
Aliwataka raia wa nchi jirani ambao wanamiliki silaha, waanze kufunga virago vyao mapema la sivyo wasimlaumu.
Alisema ana uhakika operesheni hiyo, itamaliza kabisa vitendo vya uhalifu kwenye mapori makubwa yaliyoko katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita.
Alisema silaha zinazomilikiwa kinyume na sheria, ndizo zinazotumika kutekeleza vitendo vya uhalifu ambavyo ni pamoja na utekaji wa mabasi, unyang’anyi na mambo mengine.
"Serikali kamwe haitavumilia tena vitendo vya uhalifu hasa vinavyohusisha matumizi ya silaha, Tanzania ni nchi ya amani na Serikali itahakikisha inailinda kwa gharama yoyote," alisema Kikwete.
Aliwahakikishia wananchi wa Biharamulo, kuwa operesheni hiyo itaenda sambamba na kuwaondoa wahamiaji haramu.
Kwa kipindi kirefu, mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma ni mikoa ambayo imekithiri kwa matukio ya ujambazi wa kutumia silaha, ambazo zinadhaniwa kuwa zinatoka nchi jirani.
Hivi karibuni kundi la majambazi zaidi ya 20, yaliteka mabasi matatu katika pori la Kasindaga lililoko wilayani Biharamulo na kuwanyanganya abiria mali zao zote.
Juzi Rais Kikwete, alitoa onyo kali dhidi ya watu ambao wana nia ya kuvamia mipaka ya Tanzania, kwa ni ya kuvunja amani.
Rais alitoa kauli hiyo wakati wa sherehe za kitaifa za maazimisho ya Siku ya Mashujaa katika kambi Kaboya .

CHANZO NI GAZETI LA MTANZANIA.
No comments:
Post a Comment