EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, September 8, 2013

CHOMBEZO: KITANDA CHA MAMA MWENYE NYUMBA....SEHEMU YA 07

Na Irene Mwamfupe Ndauka
ILIPOISHIA
“Haloo…”“Halo, baba Joy…”“Nini?”“Khaa! Asa mbona unapokea simu unaniulizanini..?”“Ulitaka nikuulizeje..?”“Unajua nataka kukwambia nini..?”“Wewe mwanamke wewe, usiniletee usanii mimi,we endelea tu,” baba Joy alikata simu. Mama Joy alibaki ameishika simu yake huku
mikono ikitetemeka na wasiwasi juu…“Helena,” kwa mara ya kwanza alimuita kwa
jina mfanyakazi wake huyo…
“Abee bosi…”
“Haraka sana.”
Sekunde kadhaa, Helena akawa amefika…

“Kamuite na Fuko.”
Helena alitoka hadi kwa mlinzi…
“Bosi anatuita, lakini usoni kama hayuko
sawasawa…”

“Aah! Kakwambiaje kwani?”
“Kwanza we ndiyo ulimwambia mimi nilipigiwa
simu na mumewe..?”
“Sikusema hivyo, nilisema labda alikupigia
na wewe, nilitumia neno labda.”

“Nyiye,” mama Joy aliwaita akiwa amesimama
nje ya mlango mkubwa.
“Tunakuja mama,” alisema mlinzi huku
wakitembea kwa kasi kuelekea alikosimama.
Mama Joy alipowaona wamekaribia, aligeuka
kutangulia ndani…

“Tumefika mama…”
Mama Joy aligeuka kuwaangalia kisha akakaa
kwenye kochi…
“Nani kati yenu ni mnafiki kwangu..?”
Wote wawili waliangaliana kwa nyuso zenyen
wasiwasi…

“Nauliza nani kati yenu ni mnafiki
kwangu..?” safari hii mama Joy aliongea huku akipandisha sauti juu…
“Labda mwenzangu bosi, mimi siwezi kuwa
mnafiki kwako, hata wewe bosi unajua, ningekuwa mnafiki mzee aliponiuliza uko
na nani si ningesema upo na mzoa taka na pia ningesema na mimi niliamkia
kwako…”

“Wewe Helena ndiyo mnafiki siyo..?”
Mfanyakazi huyo alitulia kwa muda akimkazia
macho bosi wake kisha akasema…
“Mimi si mnafiki kwako bosi, ina labda
dhamira inakusumbua…”
“Dhamira inanisumbua..?”
“Ndiyo bosi…”
“Una maana gani..?”
“We bosi unajua mwenyewe, sisi na wewe tuko
kwa muda gani, lakini leo hii tuje kuanza unafiki kwako ni kweli..?”
Mama Joy alitulia kwa muda akitafakari,
kisha akawaambia…
“Ondokeni zenu.”
 
***
Siku ya pili, Helena alikuwa akinywa chai
jikono wakati simu yake ilipoita. Alikimbilia kuangalia kwenye kioo ni nani
aliyepiga…

“Mh!” aliguna kwanza. Alikuwa baba Joy…
“Shikamoo bosi…naomba utume meseji hali
mbaya sana wenzio huku nyumbani,” alipomaliza kusema akakata simu.
Baba Joy alihema kwa kasi akijiuliza maswali
mengi. Alijikuta akiyarudia yale maneno ya mfanyakazi wake wa ndani…
“Shikamoo
bosi…naomba utume meseji hali mbaya sana wenzio huku nyumbani…”

“Kunaweza kuwa kumetokea nini?” alijiuliza.
Pia akajiuliza atume meseji au asitume?
Baada ya kuwaza na kuwazua kama dakika tano,
aliamua kutuma meseji…

“Kuna nini kwani?” baba Joy aliituma meseji
hiyo. Akakaa akisubiri majibu…
“Mkeo kama ameshtuka ulivyonipigia simu,
lakini hajaonesha kuamini ila kama anataka kuamini. Tuma meseji tu.”
Baba Joy alikaa kwa muda kisha akamtumia
meseji…
“Mimi narudi leo, niko njiani hapa tayari.
Nitafikia mahali, mzoa taka akija tu, niambie.”
“Sawa bosi wangu.”
 
***
Baba Joy aliendesha gari kwa kasi huku
kichwa chake kikiwa kimejaa mawazo kibao, hasa ya wivu wa mapenzi. Hapo alikuwa
akipita Chalinze…
“Iko siku kila kitu kitakuwa wazi,” alisema
moyoni.

Mara simu yake iliita, akaangalia kwenye
skrini kisha akasonya. Alikuwa mkewe ndiyo maana alisonya, moyoni alitamani
namba aibadilishe, badala ya kuwa My Wife, iwe Malaya wa Mjini…
“Nini?” baba Joy aliuliza kwa sauti iliyojaa
machugu…
“Khaa! Yaani unapokea simu yangu na
kuniuliza nini…”
“Sema unachotaka kuniambia, kama vipi kata
simu…”
“Nakuuliza uko wapi kwani?”

“Arusha Mjini…”
“Ha! Hurudi leo..?”
“Kesho,” baba Joy akakata simu.
Mama Joy alihema kwa kasi. Alijua mambo
yameharibika, lakini alijipa moyo kwamba Mungu mkubwa!
Kisa cha mama Joy kuulizia hayo, alijua mzoa
taka angefika muda wowote ule kwani jana yake alipoondoka alimwambia asikose
kuja kesho.
Alitoka hadi getini…
“Fuko…”

“Ndiyo bosi,” Fuko aliitika kwa heshima
zote…
“Hakuna mgeni wangu..?”
“Hakuna bo…”
“Ngo ngo ngooo,” geti kubwa liligongwa…
“Labda huyo…”
“Hebu fungua.”
Fuko alifungua geti, macho ya mama Joy
yalikuwa makini kutaka kujua ni nani anaingia maana nyumba yake huingia watu
wengi…

“Shikamoo mama,” alikuwa mzoa taka bwana!
Siku hiyo alilipuka kwa suruali ya ‘jinsi’
ya mtumba na t-shirt pia ya mtumba iliyoandikwa kifuani I AM NO BODY! Nguo zote
hizo alitokelezea nazo bila kuzifua. Ile 50,000 aliyohongwa na mama Joy jana
yake ndiyo alifanyia shoping hiyo.
Mama Joy alianza kwa kuachia tabasamu kabla
ya kuitikia shikamoo hiyo, alimkazia macho mzoa take…
“Kofu…”
“Naam mama,” mzoa taka aliitika akiwa
ameshika fuko mkononi…
“Umependeza sana leo baba…”
“Asante mama.”
Kifupi, mama Joy alitokea kumpenda sana mzoa
taka kuliko mlinzi kwa sababu moja kuu. Mzoa taka alikuwa akimbeba mpaka juu ya
mlima wakati mlinzi kila alipokuwa akikaribia mlima alishidwa na kurudi nyuma.
Mama Joy alimshika mkono mzoa taka na kwenda
naye ndani, sebuleni lakini alipofika mlangoni, mzoa taka huyo aliweka pembeni
fuko lake…
“Hebu njoo wewe,” alimuita mfanyakazi wake…
“Hujambo kijana?” mfanyakazi alimsalimia
mzoa taka.
“Sijambo, shikamoo.”
“Marahaba…”
“Hebu mpe huyu juisi au maziwa ya moto kama
yapo.”
 
***
Baba Joy alikuwa akipita Mizani ya Kihaba,
meseji ya Helena ilipoingia kwenye simu yake…
“Mwenzio mzoa taka ameingia sasa.”
Baba Joy alisukuma mafuta kwa kasi ya ajabu,
baadhi ya magari yaliyokuwa yakitoka kwa mbele yake yalipisha pembeni yakiamini
kuna tatizo.
Ndani ya dakika ishirini tu, baba Joy
alifika nje ya geti la jumba lake la kifahari, akasimama huku mlinzi akiwa
hajui kama bosi wake yuko nje. Alimtumia meseji Helena…
“Bado yumo ndani?”

“Yumo. Walikuwa sebuleni, sasa wameenda
chumbani kwako wenzio. Da! Mzoa taka bosi yupo kwenye kitanda cha mama mwenye
nyumba. We ukifika Dar njoo hadi nyumbani kwako.”
Baba Joy alitamani kupaa. Hakutaka kupiga
honi ili afunguliwe geti, akafungua mlango na kushuka.
Alipofika getini alilisukuma. Kwa bahati
njema, baada ya mzoa taka kuingia, mlinzi alisahau kulifunga geti hilo kama
ilivyo kawaida yake…
“Ha! Shikamoo bosi…mi sihusiki lakini.
Halafu tulimwambia mama hakutusikia,” alisema mlinzi.
Baba Joy alimpuuza na kutembea kwa kasi
kwenda ndani. Hakushuka na brifkesi wala kitu chochote kile kingine.
Alipofika kwenye mlango mkubwa alishtuka
kwanza kwa kuona fuko chafuchafu la mzoa taka.
“Huyu mwanaharamu leo namtoa ubongo, ndiyo
dawa pekee,” baba Joy alisema moyoni akiwa sebuleni sasa. Akakumbuka kuwa,
aliposhuka alisahau bastola kwenye gari lake, akairudia.
Mlinzi alishangaa sana kumwona bosi wake
akitoka mbio…
“Kuna nini bosi, mbona unakimbia hivyo?”
“Shii,” baba Joy alimkataza mlinzi kwa
kuweka kidole kwenye midomo.
Sauti ya mlinzi ilimfikia mama Joy kule
chumbani, akashtuka kidogo...
“Mh!” aliguna…
“Vipi?” mzoa taka alimuuliza…
“Mlinzi wangu sijui anaongea na nani?”
“Si kuna mama mwingine anafanya kazi ndani
kwako…”

“Ee, labda huyo.”
Kwa bahati mbaya sana, mama Joy aliisikia
sauti ya mlinzi wake lakini hakujua alichokuwa akikiongea. Aliachana na mambo
ya nje kwa mlinzi na kumgeukia mzoa taka…
“Baby wangu, leo itakuwa kama jana..?”
“Kuhusu nini..?”
“Mambo yetu…”
“Yapi..?”

“Aaah! Nataka tukimalizana mimi na wewe
nisimfikirie mwanaume mwingine tena leo.”
“Wewe tu, mimi mbona niko poa wangu.”
Mama Joy alimshika mzoa taka, akamvutia
kwake na kumuomba denda kwa ishara. Lakini ghafla machale kama yalimcheza,
alichukua simu ya mezani na kupiga getini…
“Halo getini hapa, Fuko naongea…”
“Nimesikia sauti yako ja juu sana, ulikuwa
unaongea na nani?”
“Siyo mimi mama,” mlinzi alijibu…
“Una uhakika..?”
“Ndiyo bosi.”
Mama Joy akakata simu.
 
***
Baba Joy alisukuma geti, akazama akiwa na
bastola mkononi…
“Ili aniheshimu lazima nimbandue jicho la
kushoto,” alisema moyoni baba Joy.
 
***
Mama Joy na mzoa taka wake, walizama katika
denda kiasi kwamba, walikuwa wakichuruzisha mate. Muhemko wa mama Joy ndiyo uliosababisha
mzoa take asimcheleweshe, akamshika na kumpindulia kitandani sasa…
“Waooo,” alisema mama Joy akijifanya
anasikia raha.
 
***
Baba Joy alijiuma kidole akakunja uso.
Alikumbuka mlango wa gari haukufungwa na ndani mlikuwa na fedha nyingi sana zikiwa
waziwazi, akageuza na kutoka.
Wakati anatoma alibamiza mlango mkubwa wa
sebuleni hali iliyomfanya mkewe, mama Joy agundue kuwa kuna mtu ama ameingia
sebuleni kwake au ametoka.
“Na lazima mtu huyo atakuwa si mlinzi, maana
mlinzi hawezi kuingia sebuleni kwangu bila ya ruksa,” alisema moyoni mama Joy,
akatoka kitandani, akachukua khanga na kujifunga maana tayari alishavua nguo na
kubaki kama alivyoingia duniani kwa mara ya kwanza…

“Kama ni mlinzi leo atanitambua. Ina maana
kuwa na yeye kwa siku moja tu ndiyo ameshapata tiketi ya kufanya anavyotaka?”
Alipofika sebuleni, alishtuka kumwona mume
wake akiingia getini tena akiwa kasi…
“Ooh! Mungu wangu nimekwisha mimi,” alisema
mama Joy na kukimbilia chumbani. Alimkusanya mzoa taka na nguo zake na kumvuta
kutoka naye hadi jikoni ambako mfanyakazi alikuwepo akiendelea na shughuli
zake.

Mfanyakazi huyo alijifanya ameshtuka sana
kuliona tukio hilo, lakini alikuwa analijua litakuwepo tu.
Mama Joy baada ya kumtelekeza mzoa take
jikoni alirudi chumbani haraka, akaweka shuka vizuri na kujifanya amekaa.
Mlango ulisikumwa kwa nguvu, baba Joy
akazama ndani huku akihema kwa kasi ya ajabu…
“Yuko wapi?” ndiyo swali alilomuanza nalo
mkewe…
“Yuko wapi nani?”
“Huyo mzoa taka wako…”
“Mzoa taka wangu! Yupi huyo?” mama Joy
alijibalaguza ingawa ukweli alikuwa akiujua. Alikuwa akitetemeka maana mumewe
alishika bastola.
 
***
Kule jikoni, Helena alihisi mambo
yataharibika zaidi kwa ndoa ya mabosi wake, alichofanya, alimchukua mzoa taka
kumpeleka nje kwa njia ya uani.
Mlinzi getini alitaka kulipua bomu, lakini
Helena akamuwahi…
“Unataka kusema nini, wewe je, hujawahi
kulala kwa mama? Sema na mimi nikusemee.”
Mzoa taka alipitishwa, akasepa zake akiacha
lile fuko chafu la takataka.
 
***
“Mimi si mwendawazimu eti niulizie nani
halafu pasiwepo mtu, nina ushahidi wote kwamba yupo,” alisema baba Joy huku
akiinama kwa lengo la kuchungulia chini ya kitanda…
Mama Joy alibaki kimya kwani aliamini
kuingiza maneno mengi kusha aende akamnase jikoni angewamaliza wote, hata yeye.

Baba Joy alipoona mvunguni mwa kitanda hola,
alilifuata kabati la nguo, akafungua humo, lakini hamkuwa na kitu, akaenda
chooni ambako pia hakuona kitu.
Alitoka kwa hasira akimwacha mkewe chumbani
hadi jikoni, hola. Akaenda kwenye vyumba vinne vya wageni, hamna kitu. Akenda chumbani
kwa mfanyakazi…

“Si kawaida yangu kuingia humu lakini leo
nimelazimika,” alisema baba Joy akitoka. Aliamua kwenda uani kwa nyuma ambapo
ili afike huko lazima apitie jikoni, akakutana na Helena akiwa anaingia kutoka
kumsindikiza mzoa taka…
“Hujambo..?”
“Sijambo bosi, habari za safari..?”
“Nzuri, mbona sijamwona..?”
“Hayupo ndani..?”
“Sijamwona, nimekuja hadi chumbani kwako
lakini hamna kitu.”
“Kha! Atakuwa amekwenda wapi sasa? Aliingia
naye lakini.”

“Au uliona vibaya, si ajabu aliingia kuzoa
taka na kuondoka zake. Lakini hapana, huyu atakuwemo humuhumu ndani maana
mlangoni nimekuta fuko lake chafu, linanuka,” alikandia baba Joy huku akitoka
uani ambako pia hakufanikiwa kumwona mzoa taka. Hapo, bado mkononi alishika
bastola yake tayari kwa kumtegua shingo mwizi wake.
Baba Joy alikwenda hedi getini…
“Fuko…”

“Yes boss…”
“Kuna mtu katoka baada ya mimi kuingia..?”
“Muda huu..?”
“Ndiyo muda huu…”
“Unataka
kusema nini, wewe je, hujawahi kulala kwa mama? Sema na mimi nikusemee.”
Mlinzi alipokumbuka maneno hayo ya Helena,
alijikuta akifunga kinywa chake…
“Sijaona mtu bosi…”
“Una uhakika..?”
“Kabisa kabisa bosi wangu…”
“Sasa funga geti, usifungue mtu kuingia wala
kutoka hadi nitakaposema mimi.”

”Sawa bosi,” alisema Fuko kwa utii wote huku akimwangalia
baba Joy kwa macho ya kuibia. Kama baba Joy angekuwa makini angegundua
jambo geni kwenye macho ya Fuko…
“Nikisikia
amepita mtu hapa mimi na wewe wewe na mimi.”

“Hapiti mtu bosi, si kuingia si kutoka.”
Baba Joy alikwenda ndani, alikagua kila sehemu ambayo
aliamini inaweza kuwa na maficho ya mtu lakini hakuweza kumwona mzoa taka wala
muokota makopo.
Alikwenda kwenye ukuta pembeni kabisa kisha akampigia
simu Helana.
”Haloo bosi...”
”Helena...”
”Abee bosi...”

”Hivi mzoa taka hakutoka kweli?”
”Mimi sina kumbukumbu nzuri bosi zaidi ya kumwona
akiingia.”
”Kutoka hukumwona..?”
”Ukiwa jikoni si rahisi bosi kumwona.”
”Oke sawa, ndani hayupo. Oke kwaheri, lakini asante kwa
ushirikiano wako.”
”Sawa bosi wangu.”

Baba Joy alirejea sebuleni akatoa kiti na kukaa nje ya
nyumba eneo ambao hakuna mtu anayeweza kuingia ndani kwake kupitia getini nila
yeye kumwona kwa macho...
”Chai
taayri,” mkewe mama Joy alimwambia…
“Niletee
hapahapa.”
Chai
ilipelekwa pale nje, mama Joy moyoni alikuwa akichekelea kwani alijiona ni
mshindi. Baada ya kumwekea chai mumewe aliingia ndani akaenda jikoni…
“Helena…”
“Abee
bosi…”
“Mzoa
taka alitoka?”
“Nilimtoa
mama, si unasema mi mnafiki, lakini hebu ona wema niliyokutendea…”

“Ulimtoaje?”
“Mpaka getini…”
“Mlinzi
hakumuona?”
“Ndiye
aliyemfungulia mlango…”
“Akasemaje?”
“Alitaka
kumkatalia asitoke ili baba amuone…”
“Sasa,
ikawaje?”

“Nilimwambia
afanye hivyo halafu mimi niseme hata yeye alipolala na wewe usiku wa juzi…”
“Una
uhakika..?”
“Niliwaona
mama…”
“Kelele…”
“Basi
bosi…”
“Sasa
sikia, hakikisha baba Joy hapati taarifa potofu kuhusu mimi na mzoa taka,
akikuuliza simamia uongo, mwambie kwamba alikuja akazoa taka na kuondoka zake…”
“Lakini
bosi…”
“Lakini
nini sasa..?”
“Kuna

kitu kimoja hujakijua…”
“Kama..?”
“Fuko la
mzoa taka…”
“Limefanyaje?”
“Huna
habari..?”
“Ningekuuliza
Helena..?”
“Liko
mlangoni nje pale…”
“Mh!
Kweli..?”
“Hata
sasa lipo…”
“Baba
Joy ameliona..?”

“Amekaa nalo jirani, si amekaa nje..?”
”Ndiyo... lakini bado uongo utashika nafasi yake, utasema
alichukua fuko jingine zuri alipewa na mama.”
”Si mzee atakasirika kutoa fuko jipya zuri kumpa mzoa
taka asiyempenda..?”
”Afadhali uovu huo kuliko wa kitandani...”
”Sawa bosi.”
 
***
Mzoa taka alifika kijiweni akiwa anahema kwa kasi ya
ajabu...
”Msela
vipi?” msela mwenzake alimuuliza…
“Ni
noma, nusu nidakwe…”
“Na
nani?”
“Mwenye
mji, ye kazuka tu bila mawasiliano na mkewe…”
“We

ulikuwa wapi?”
“Si
kwenye kitanda…”
“Cha
nani..?”
“Cha
mama mwenye nyumba, nikazama nikaibuka, nilipofika getini eti ulinzi shirikishi
naye anataka kuniwekea wingu, ningemtoa roho ujue, mi sioni noma kulala jela,
maisha yenyewe nimeshachoka nayo.”
 
***
Baba Joy
baada ya kumaliza kunywa chai, alimuita mlinzi wake, Fuko…
“Hebu
vuta kiti ukae hapa nataka kusema na wewe…”
“Sawa
bosi.”

Baada ya
mlinzi kukaa, baba Joy alimwangalia kwa macho makubwa kisha akachukia…
“Huu mfuko mchafu ni wa nani..?”
”Mzoa taka bosi...”
”Yuko wapi..?”
”Sijajua bosi...”
”Una maana gani..?”
 
”Nina
maana sijajua aliko kwa sasa...”
“Mimi
nahisi kazi imekushinda…”
“Hapana
bosi, haijanishinda…”
“Sasa
kwanini usijue nani kaingia nani katoka wakati we upo getini...?”
“Nisamehe
bosi…”

“Sasa
sikia, ili uendelee kuwa kazini nijibu swali langu moja tu…”
“Sawa
bosi…”
“Mzoa
taka alipoingia alipitia wapi?”
“Pale getini bosi…”
“Alitoka..?”

“Sijamuona bosi…”
”Sasa nakupa kazi, mimi nitaangalia geti, wewe nenda
ndani, zunguka kote hakikisha unampata mzoa taka kisha mlete hapa kwangu,
sawa?”
”Sawa bosi.”
Mlinzi Fuko alikwenda ndani, alianza kwa kufikia jikoni
ambako alimkuta Helena...

”Leo balaa,” alianza kwa kusema...
”Balaa kivipi?”
”Sai bosi...”
”Bosi gani..?”
”Mwanaume...”
”Kafanyaje?”
”Mh! Eti kaniambia niingie huku ndani, nimtafute mzoa
taka kila sehemi hadi nimpate kisha nimpeleke kwake...”

”Ah! Hilo tu...”
”Unasema hilo tu sasa nitampataje?”
”We zuga huku wee, kisha nenda kamwambie hujamuona,
unahisi ulipokuwa ndani yeye katumia mwanya huo kutoka getini...”
”Mh! Unajua yeye yuko wapi?”

”Si sebuleni..?”
”Nani kasema, amekaa getini. Kasema anashika nafasi yangu
ili mtu asiingie wala kutoka.”
Mara, mama Joy alitokea jikoni...
”Fuko unafanyaje hapa..?”

”Bosi kuna tatizo kubwa...”
”Ni tatizo gani linakufanya uache lindo na kuja kukaa
hapa, geti unamwachia nani?”
”Getini yuko bosi...”
”Yuko bosi! Una maanisha baba Joy..?”

”Ndiyo bosi...”
”Kwanini..?”
”Aliniita, akaniuliza kama nilimwona mzoa taka akiingia,
nikamjibu ndiyo, akaniuliza nilimwona akitoka? Nikamjibu sijamwona, ndiyo
akasema nimtafute humu ndani hadi nimpate, yeye amekaa getini kuchukua nafasi
yangu.”

Mama Joy alivuta pumzi, akawa mambo mengi. Aliwaza kuwa,
mlinzi wake alikuwa sahihi au si sahihi kumjibu mumewe kwamba, mzoa taka
aliingia...

”Lakini si alishajua aliingia, sasa labda kwenye kutoka,
angemjibuje, alimuona akitoka au hajamuona...?”
”Oke, wewe rudi, mwambie Helena amekwambia mlinzi
alitoka...”

”Hapana bosi, hata mimi nilimwambia sijamwona akitoka...”
”Alikuuliza saa ngapi?”
”Muda si mrefu bosi...”
”Alikuja jikoni..?”
”Ndiyo bosi.”

”Mh! Baba Joy naye kwa kubana...”
”Ni kweli bosi, amekubana sana, huna ujanja,” alisema
mlinzi huku akicheka hali iliyomkera sana mama Joy...
”Kwako ni furaha na amani au?” mama Joy alimuuliza
Fuko...

”Hapana bosi, unajua mzee amechezwa na machale na inabidi
utengeneze sana ili asiendelee kukuchunguza, ni hatari kwako...”
”Umeyatoa wapi maneno hayo..?”

”Ni mawazo yangu tu bosi...teh! Teh! Teh!”
Mama Joy alitoka kwa kasi na kwenda chumbani kwake. Kule
nyuma, Helena na Fuko walijiuliza...
”Sasa bosi anapoondoka na hasira anategemea nini? Yeye
ndiyo alitakiwa kushauri nini kifanyike ili kuondoa hii hali,” alisema Fuko...

”Sasa ndiyo imetokea wewe tafuta njia...”
”Sina njia, labda nisaidie wazo.”
Helena alitulia kwa muda kisha akasema...
”Sikia, mfuate bosi getini, mwambie umekagua kila mahali
hujamwona mzoa taka. Lakini una wasiwasi na chumbani kwake maana ni huko tu
ndiko hujafika...”

”Mh! Je, kama na yeye akienda na kukagua kila mahali huko
chumbani, hata chini ya kitanda, kabatini, chooni, bafuni kote asipomwona mzoa
taka si atajua amepita getini..?”

”Mwambie kuna wakati mama alikutuma dawa ya meno, labda
alitumia muda huo wa kukutuma kumtoa mzoa taka...”
”Eee, sawasawa, hapo nakubaliana na wewe,” alisema mlinzi
na kutoka jikoni. Alirudi getini...

”Yuko wapi mzoa taka, fuko lake chafu bado liko hapa na
wewe nimekwambia lazima umlete kwangu,” baba Joy alisema...
”Bosi, nimemsaka kila mahali lakini wapi! Nina wasiwasi
na chumbani kwako kwa sababu ndiko mahali pekee sijafika...”
”Chumbani nilimtafuta hadi ndani ya kabati la nguo,
hayupo. Bado kesi iko kwako. Lazima alipita hapa getini, je alipitaje?”
”Ee bosi nina wasiwasi na jambo moja...”
”Lipi hilo..?”

”Labda alipita wakati bosi mdogo aliponituma dawa ya meno
dukani.”
”Alikutuma dawa ya meno?”
”Ndiyo bosi...”
”Ulitumia dakika ngapi kwenda na kurudi?”

”Kama kumi bosi, maduka ya kule chini karibu na
barabara.”
Baba Joy alitingisha kichwa kama kukubaliana na maneno ya
Fuko...
”Oke...sawa, ni nimekuelewa vizuri, endelea na kazi,”
alisema baba  Joy.
Alisimama mlango mkubwa na kumwita mkewe...

”Mama Joy...”
”Abee.”
Sekunde kadhaa mbele, mama Joy alisimama mbele ya
mumewe...
”Abee...”
”Hili fuko la taka hapa chafuchafu vipi?”
Usikose sehemu ya 08 siku ya jumatano wiki ijayo na Irene Mwamfupe Ndauka.

1 comment:

  1. asante kwa story nzuri. Lkn mbona story ya some text missing hujaimalizia?












    ReplyDelete

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate