EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, July 24, 2013

Kivazi chazua sokomoko kanisani

KIVAZI cha ndugu wa maharusi, kimesababisha patashika katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Peter, baada ya Paroko Msaidizi wa Kanisa hilo, Padri Paulo Haule, kusitisha ibada mpaka mhusika atoke akavae vizuri.

“Ninatoa dakika 10 kwa aliyeingia na mavazi ambayo hayatakiwi kanisani humu kutoka mara moja akavae vizuri, la sivyo ndoa yao haitafungwa,” alisema Padri Haule wa Kanisa hilo lililoko Oysterbay, Dar es Salaam.

Awali vurugu hizo zilizotokea Jumamosi iliyopita, zilianzia nje, wakati Katekista wa Parokia hiyo, Yohane Maboko, alipotangazia wanandoa na ndugu zao waliokuwa mabega wazi au kuvaa nguo fupi, kutafuta nguo za kujifunika au wasiingie kabisa kanisani.

Maharusi walikubali kutekeleza ombi hilo, wakavishwa vitambaa mabegani vya rangi tofauti na gauni jeupe la harusi, wakaruhusiwa kuingia kanisani, tayari kufunga pingu zao za maisha.

Hata hivyo, mmoja wa ndugu wa maharusi hao ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alipotaka kulazimisha kuingia na kivazi chake cha mabega wazi, alizuiwa na Katekista Maboko. Katekista huyo alimfuata mwanamke huyo ili kumrudisha akavae vizuri, lakini aliibua zogo na kulazimisha kuingia na vazi hilo.Zogo hilo lilipoendelea, wanandugu waliingilia kati, wakitetea vazi hilo ambapo mmoja wa wanandugu, alimvua miwani Katekista Maboko na kuipiga chini ikavunjika huku yeye na wenzake wakimtolea maneno makali ya kumtaka asimzuie ndugu yao kuingia kanisani. Wakati ndugu hao wakimdhibiti Katekista Maboko, mwanamke huyo alitumia mwanya huo na kupenya hadi ndani ya Kanisa, ambamo Padri Haule, alikuwa akijiandaa kuanza ibada.

Taarifa kwa Padri Baada ya Padri Haule kupata taarifa, alitangaza kuwa ndoa ya maharusi wa msichana huyo, haitafungwa hadi awe ametoka. Licha ya Paroko kutangaza hivyo, bado ukaidi uliendelea jambo lililomfanya Katekista Maboko kumfuata tena dada huyo na kumwamuru atoke nje, ambapo aliendelea kupinga na baadaye akatekeleza amri hiyo ya Paroko. Baada ya hapo shughuli za kufungisha ndoa ziliendelea kwa amani na utulivu hadi mwisho maharusi wakatoka kwenda kuendelea na mambo mengine.

Akizungumza na gazeti hili, Katekista Maboko alisema waumini hao walikiuka maadili ambayo Kanisa lina wajibu wa kulinda na kuyasimamia ili waumini wake wayafuate. Alisema miwani yake iliyovunjwa ilikuwa na thamani ya Sh 90,000 na baada ya ibada hiyo, aliyetenda kosa hilo alimwendea na kumwomba radhi na kulipa Sh 50,000 na kuahidi kumalizia kiasi kilichobaki wakati wowote.

Maboko alisema uvaaji wa mavazi yasiyotakiwa kanisani hapo, umekuwa ukipigiwa kelele mara kwa mara, na hata katika mafundisho ya ndoa huambiwa lakini ukaidi unaendelea. “Maharusi wakati wa mafundisho ya ndoa tunawaambia kuhusu mavazi yao na hata ya ndugu zao watakaowasindikiza kanisani, kuwa wavae kistaarabu lakini hawasikii,” alisema Katekista Maboko.
 
 Makanisa mengi siku hizi yamekuwa yakipiga marufuku uvaaji wa nguo fupi na zinazoacha mabega wazi kwa wasichana na wanawake, wakati wa ibada za kawaida na za ndoa.
CREDIT : HABARI LEO

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate