NANI amenuna? Hayawi… hayawi sasa yamekuwa! Mwigizaji mkongwe Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ hatimaye amefunga ndoa ya uzeeni akiwa na umri wa miaka 46.
Tukio hilo lililopambwa na cherekochereko za kufa mtu, lilijiri
Jumamosi ya Julai 20, 2013 ambalo lilianzia kwenye Kanisa la Mt. Joseph
lililopo Posta, Dar ambapo Natasha alifunga ndoa na mwanaume aitwaye
Alex Humba Lumila.
Baada ya ndoa hiyo kufungwa kanisani hapo, mnuso ulihamia kwenye Ukumbi wa Magereza uliopo Ukonga, Dar.
Wakiwa ukumbini, mastaa wa Kibongo na wageni waalikwa waligonga ‘mpunga’ na vinywaji vya kila aina ambavyo vilikuwa vya kumwaga.
Wakiwa ukumbini, mastaa wa Kibongo na wageni waalikwa waligonga ‘mpunga’ na vinywaji vya kila aina ambavyo vilikuwa vya kumwaga.
Gazeti hili lilipata nafasi ya kuzungumza na Natasha baada ya kufunga ndoa ambapo alisema kuwa siku hizi uzee unaishia Chalinze
kama unaelekea Dar na anachojua yeye ni kuwa hajawahi kuolewa na hiyo ndiyo ndoa yake ya kwanza.
kama unaelekea Dar na anachojua yeye ni kuwa hajawahi kuolewa na hiyo ndiyo ndoa yake ya kwanza.
“Ninamshukuru Mungu kufanikisha siku yangu, sasa nahitaji kufurahia
maisha ya ndoa. Mungu atutangulie tuishi milele,” alisema Natasha ambaye
alipambwa na kupambika katika saluni mashuhuri ya kuremba mastaa ya
Partners Wedding iliyopo Sinza Kwa Remmy, Dar.
No comments:
Post a Comment