POLISI wapatao sita Jumamosi iliyopita walivamia nyumbani kwa staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu maeneo ya Kijitonyama kwa lengo la kumkamata kufuatia kesi iliyofunguliwa katika Kituo cha Polisi Kawe jijini Dar.
Baada ya kesi hiyo yenye jalada KW/RB5988/2013 SHAMBULIO kufunguliwa kituoni hapo Julai 6, mwaka huu mishale ya saa 5 asubuhi, maafande hao wakiwemo wa kike wawili wakiwa wamevaa kiraia walifika mtaa anaoishi staa huyo na kuufunga kabla ya kwenda kugonga katika geti la nyumba yake.
Mara baada ya kugonga geti hilo, alitoka mwanaume aliyefahamika kwa jina la Petman, alipoulizwa kuhusu Wema, alijiumauma huku kijasho kikimtoka kabla ya kutoa jibu la kwamba hakuwepo.
Majibu hayo hayakuwaridhisha polisi hao ambapo walilazimika kuzuia kila gari lililokuwa linatoka getini hapo wakiamini huenda Wema angetolewa kiujanjaujanja.
Maafande hao waliomba namba ya simu ya Wema na walipompigia alisema yuko Zanzibar, kesi hiyo anaijua na atakaporejea atajisalimisha mwenyewe polisi.
CREDIT: GLP. |
No comments:
Post a Comment