RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba
amefunguka kuwa kama wasanii wataendelea na tabia waliyonayo kwa sasa
watapukutika kama maua na itabakia miti tu.
Akichezesha taya na paparazi wetu, Mwakifwamba alisema kutokana na
wasanii wengi wa filamu kuwa na tabia ya kuzungukana kimapenzi na
kuwekeana ‘mabifu’ kwa sababu ya kuchukuliana wapenzi na kurogana basi
kwa hali hiyo watapukutika kama maua na kubaki miti kwani magonjwa ni
mengi.
“Yaani kama wasanii wataendelea na tabia yao hii chafu ya
kuzungukana kimapenzi yaani unakuta mwanaume mmoja anakuwa na uhusiano
wa kimapenzi na wasanii wa kike zaidi ya watu hali itakuwa mbaya kwani
kama mmoja ana ugonjwa hatari wa Ukimwi atawamaliza wenzake wote hali
ambayo itasababisha kupukutika kama maua na kubaki miti tu,” alisema.
Hata hivyo, Mwakifwamba aliwataka wasanii wa filamu kuachana na tabia
hizo kwani hali ya dunia ni mbaya kwa sasa pia wajitambue wao ni kioo
cha jamii kinachotazamwa na wengi.
Credit:GLP
No comments:
Post a Comment