MLIMBWENDE aliyewahi kung’ara katika Shindano la Miss Kiswahili 2009,
Rehema Fabian anadaiwa kuangukia kimapenzi kwa mtoto wa Balozi wa
Nigeria nchini China aliyemtaja kwa jina moja la Allen anayetaka kufunga
naye ndoa.
Akichati na Risasi Mchanganyiko, kwa njia ya mtandao,
Rehema alikiri kuwa na mwanaume huyo ambaye ni mtu mzima na kweli ni
mtoto wa balozi huyo.
“Nimechoshwa na masharobaro hivyo nimeamua
kutulia na mwanaume huyo kwa sababu nimempenda na yeye anaonekana
kunipenda,” aliandika Rehema.
Rehema ambaye kwa muda mrefu amekuwa nchini humo, alisema kwamba amekuwa akipata wanaume wanaomtumia na kumuacha lakini safari hii amepata mtu sahihi.
Rehema ambaye kwa muda mrefu amekuwa nchini humo, alisema kwamba amekuwa akipata wanaume wanaomtumia na kumuacha lakini safari hii amepata mtu sahihi.
“Tumepanga kuja
Tanzania kwa ajili ya kukamilisha mipango ya ndoa, hivyo nitarajieni
huko muda si mrefu,” aliandika Rehema na kuongeza kwamba atafanya bonge
la sherehe.
Credit:
Risasi Mchanganyiko-GLP.
Risasi Mchanganyiko-GLP.
No comments:
Post a Comment