Mikakati ya Kituo cha Faragha na Maombi ya kujenga chuo cha ufundi,
maabara na kituo cha polisi, imeanza kuzaa matunda, baada ya kufanikiwa
kukusanya Sh. milioni 70 kati ya Sh. milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa
vitu hivyo.
Fedha hizo zilichangwa katika harambee iliyofanyika katika Kijiji cha Chasimba, Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, iliongozwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika mikakati hiyo, kituo hicho kimepanga pia kujenga kumbi za mikutano na viwanja katika eneo maalum.
Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kariakoo, Eliona Kimaro, aliliambia NIPASHE kuwa licha ya kutofikia malengo, anamshukuru Mungu kwa kuwa watu wameonyesha moyo wa kuchanga ili kukamilisha kituo hicho.
Alisema kati ya fedha ziliozochangwa, taslimu ni Sh. milioni 13, huku milioni 57 zikiwa ni ahadi.
Aliwataka waumini kuendelea kuchangia ujenzi huo na kuwashukuru wanausharika wa Kariakoo kujitoa na kununua eneo hilo lenye ukubwa wa hekari 120 kwa Sh. milioni 46.
CREDIT: NIPASHE

No comments:
Post a Comment